Ugonjwa unaoambukiza kama UKIMWI, kati ya watu 100, Nane wanao
Hospitali
ya Taifa Muhimbili inatarajia kuanza kufanya uchunguzi wa Virusi vya
homa ya Ini (Hepatitis B) na kutoa tiba bure kwa wagonjwa
watakaobainaika kuwa nao kwa kutumia dawa ya Tenefovir katika kipindi
cha miaka mitano ijayo kuanzia tarehe 1 December 2016.
Tanzania
itakua nchi ya pili ukanda wa Afrika Mashariki kuanza kutoka huduma ya
uchunguzi na matatibu ya ugonjwa wa Ini baada ya Rwanda ambayo
imeshaanza udhibiti wa tiba ya ugonjw ahuo.
Kwa mujibu
wa Dr. John Lwegasha ambaye ni Daktari bingwa wa magonjwa ya Ini na
Matumbo kutoka Hospitali ya Muhimbili amesema nchini Tanzania kati ya
watu 100 watu nane wameambukizwa Virusi vya homa ya Ini.
0 maoni:
Post a Comment