Warajisi walalamikiwa kuto kuwa makini chanzo vyama vya ushirika kufa


WARAJISI wa Vyama vya Ushirika wa wilaya nchini wamedaiwa kuwa
ni wazembe na chanzo cha vyama hivyo kufirisika kwa kuto kuwa wasimamizi wazuri
na kushituka vyama hivyo mimesha baki vitupu na kukaribia kufa.
Hayo yanaibuliwa na
wanasakosi wa chama cha ushirika cha wafanyabiashara   Njombe
ambacho kimefirisika na fedha za wanachama huku kikubakia na madeni ya zaidi ya
milioni 800 za wanachama na fedha kutoka taasisi za kifedha.

Katika mkutano wa Dharula uliowakutanisha wananchama na
warajisi wa Kitaifa na mkoa wa Njombe wa kusoma taarifa ya Mapto na Matumizi ya
Chama Hicho zinaibuka lawama kwa warajisi
Walioweka fedha kwa malengo ya kusomesha na kuibua miradi yao
wanasikitika kushindwa kufikia matarajio ya kuweka fedha katika chama hicho.
Bodi ya chama hicho inadaiwa kukopesha fedha bila kufuta
vigezo vya kutoa mkopo na kusababisha Saccos hiyo kufirisika ambapo mikopo hiyo
ilitolewa kinyume cha sheria.
Kutokana na kuibuka kwa hayo Bodi ya chama hicho inavunjwa na
kaimu Mrajisi Msaidizi wa udhibiti wa vyama vya ushirika wa kifedha Tanzania na
bodi mpya inaundwa ili kufuatilia fedha hizo.

from Blogger http://ift.tt/2fNqFwf
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment