Bodi ya Chakula
Dawa na Vipodozi Zanzibar (ZFDB) imeangamiza zaidi ya tani 62 za vyakula
vibovu na vilivyopitwa na wakati katika zoezi lililofanyika Kibele Mkoa
Kusini Unguja.Mkuu wa Idara ya Biashara na Uendeshaji wa ZFDB Ndugu
Abdulaziz Shaib Mohd amesema bidhaa hizo mbovu zinatokana na tabia ya
baadhi ya wafanyabiashara kujenga matumaini ya kuingiza faida kwa
bidhaa wanazouza bila kuangalia usalama wa bidhaa hizo kwa afya za
watumiaji.
Amewataka wafanyabiashara kuwa wazalendo kwa wananchi wenzao na kujuwa kwamba biashara mbovu ama zilizopitwa na wakati ni sumu na zinaweza kudhofisha afya zao.Mkuu wa Idara ya Chakula bibi Aisha Suleiman amesema mchango mkubwa wa raia wema ndio uliofanikisha kugundulika bidhaa mbovu na zilizopitwa na wakati katika maduka na maghala mbali mbali.
Hata hivyo amewataka wananchi kujenga tabia ya kuchunguza tarehe ya kumaliza muda bidhaa wanazonunua na wanapogundua bidhaa imepitwa na wakati watoe taarifa katika Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi ili hatua za haraka ziweze kuchukuliwa.
Wakati huo huo;
Afisa Mkuu wa Idara ya Dawa na Vipodozi Ndugu Mwadini Ahmada Mwadini ,amesema vipodozi haramu vilivyokamatwa baadhi yake vina kemikali zenye sumu na hazifai kwa afya ya binadamu.Amewashauri wafanyabiashara wanaotaka kuanzisha biashara ya dawa na vipodozi kushirikiana na Bodi hiyo kwa lengo la kulinda afya za wananchi.
Dawa zilizoangamizwa katika operesheni hiyo ni mafuta ya kula lita 10,105, sukari tani 2.15, mchele tani 26, tende tani 10, bidhaa mchanganyiko za mboga mboga tani 13, dawa na vipodozi tani tatu.
0 maoni:
Post a Comment