Kocha wa Manchester United Jose Mourinho amesisitiza kuwa timu yake inaweza kumaliza katika nafasi bora zaidi kuliko ya nne kwenye Ligi Kuu ya Uingereza, maarufu kama EPL, lakini Mreno huyo amesema hataki kuiwekea malengo timu hiyo katika  msimu huu.
Jose Mourinho - Kocha wa Man United

Kwa sasa United wako katika nafasi ya sita ya msimamo wa ligi kuu baada ya kushinda michezo mitatu mfululizo, huku wakiwa pointi nne nyuma ya timu nne bora wakati wakiingia kipindi hiki cha Krismasi.

United walimaliza nje ya nafasi ya kufuzu Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya msimu uliopita chini ya kocha wao wa zamani Mdachi Louis van Gaal na Mourinho amesema kuwa hataki kuweka lengo la timu yake kumaliza katika nafasi ya nne, akisisitiza kuwa timu yake inaweza kufanya vizuri zaidi kuliko hiyo licha ya ushindani mkali.