Wizara inapanga kusambaza mitungi ya gesi ya kupikia milioni 1.2 kwa familia mbalimbali



Zaidi ya familia milioni moja nchini Kenya watafaidika na mapango wa serikali wa kuongeza matumizi ya gesi ya kupikia.

Wizara ya Nishati na Petroli imesema kwamba italipa bei ya awali ya kununua mtungi wa gesi ya kupikia kwa niaba ya familia hizo, kisha watalipa bakio baadaye.
Wizara inapanga kusambaza mitungi ya gesi ya kupikia milioni 1.2 kwa familia mbalimbali katika maeneo ya mijini na vijijini.

Kando na usaidizi kutoka kwa serikali, familia hizo ambazo zitapata mitungi ya gesi zitapatiwa muda wa kutosha wa kulipa pesa iliyosalia.

Msaada huu wa serikali ni wa mitungi ya gesi ya kilo sita.
Hatua inatarajiwa kuongeza matumizi ya gesi kupikia badala ya njia zengine za kupikia ambayo ni hatari kwa afya ya binadamu na mazingira.

Serikali inataka kumaliza matumizi ya kuni na mafuta ya taa.
Paul Mbuthi, afisa mkuu wa nishati mbadala katika Wizara ya Nishati, anasema mradi huu utatekelezwa ifikapo mwezi Juni mwaka ujao.

Matumizi ya gesi kupikia nchini Kenya imebakia chini, ambayo imechangia kupanda juu kwa gharama mitungi ya gesi.
Hazina ya Taifa ya fedha hivi majuzi iliondoa asilimia 16 ya ushuru wa bidhaa kwa gesi ya kupikia.
Hatua ambayo imesababisha ukuaji katika matumizi ya kupikia gesi.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment