Edo Kumwembe anaswa kwa unga

Image result for Edo Kumwembe
ILIANZA kama mzaha. Ilianza kama masihara. Sikutegemea. Ilikuwa wakati kipindi cha baridi kikimalizika barani Ulaya kupisha ujio wa majiraa joto, Aprili 2013.
 Unaweza kudhani ilikuwa hadithi ya kutunga lakini ni kisa kilichonitokea. Kila nikikumbuka huwa natabasamu na kuishia kucheka. Wakati mwingine mwanadamu anajikuta ghafla yupo katika mazingira mepesi yaliyojaa raha nyingi. Ghafla anakumbana na janga kubwa ambalo hakulitegemea. Inatokea.
 Ni kweli ilinitokea Aprili 25, 2013 nikiwa mapumzikoni Ulaya. Nilikuwa katika nchi ya Uswisi ambako nilikwenda kumtembelea rafiki yangu mkubwa, staa wa zamani wa Simba na timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Renatus Njohole ambaye anaishi katika Jiji la Yverdon tangu mwaka 1999. 
Awali Renatus alikuwa akicheza soka la kulipwa katika klabu ya Yverdon iliyokuwa Ligi Kuu Uswisi, 
lakini sasa anacheza daraja la tatu katika soka la ridhaa klabu ya FC Bavois huku akifanya kazi nyingine. Ni kawaida kwangu kumtembelea Renatus kwa sababu ni rafiki yangu wa karibu tangu tukiwa shuleni Jitegemee pale Kurasini mwishoni mwa miaka ya 1990. Nilisoma naye kidato cha tano na sita. Nyakati hizo alikuwa mwanafunzi, pia akicheza soka kwa ustadi mkubwa.
 Mara zote nilizokwenda Ulaya safari huwa inaanzia kwake kwanza. 
Safari hii haikuwa tofauti na safari nyinginezo, lakini nilikuwa nataka kufika mbali zaidi ya Uswisi. Nilikuwa nataka kwenda Italia kutimiza ndoto ya kufanya mahojiano na mwanasoka wa kimataifa wa Kenya, McDonald Mariga ambaye nyakati hizo alikuwa akikipiga katika klabu ya Parma kwa mkopo akitokea Inter Milan.
 Mariga alikuwa ana miaka miwili tangu aweke rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kutoka Kenya na Afrika Mashariki kucheza Ligi ya Mabingwa na kutwaa michuano hiyo akiwa na Inter Milan. Kwa nini nisimhoji Mariga? Ningemfuata kokote alipo kwa ajili ya kuandika safari yake ya soka. 
Hata hivyo, kabla ya kwenda kwa Mariga ilikuwa lazima safari ianzie kwanza Uswisi kwa kumtembelea Renatus na familia yake. Ingekuwa rahisi kwangu kusafiri kutoka Yverdon Uswisi mpaka Parma kumfuata Mariga kuliko kutoka Dar es Salaam moja kwa moja mpaka Parma. Uswisi na Italia ni nchi ambazo zinapakana katika upande wa Mashariki. 
Niliwasili Uswisi, moja ya nchi zenye baridi kali barani Ulaya kwa kutumia shirika la Ndege la Swiss Air na kutumia siku nne kukaa pamoja na familia yake. Renatus ana mke wake wa kizungu, Nadja pamoja na watoto wake watatu wote wa kiume. Baada ya siku chache za kukaa na Renatus na familia yake iliwadia siku ambayo nilipaswa kwenda Italia kwa ajili ya mahojiano na Mariga. Kwa mpangilio wa usafiri ulivyokuwa, Renatus alinishauri kwamba ingekuwa rahisi kwangu kupanda treni ya moja kwa moja kutoka katika mji unaoitwa Lausanne nchini Uswisi mpaka mji mkuu wa Italia,
 Milan kisha nichukue treni nyingine niende Parma kwa ajili ya kukutana na Mariga. Ilikuwa rahisi tu kwamba Renatus angenipeleka kwa gari kutoka Yverdon mpaka Lausanne kisha ningechukua treni. Asubuhi ya siku ambayo nilipaswa kusafiri nilichukua maamuzi ambayo sikujua kama yangenigharimu sana mbele ya safari na kuzua mkasa huu wa kusisimua.

from Blogger http://ift.tt/2lVtBOz
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment