Haya ndiyo madhara wanayoyapata wafanyakazi wa saluni wapakao rangi za kucha


Wanawake wengi hawawezi kutoka nyumbani bila kuhakikisha kucha zao zimeng’aa kwa rangi nzuri na zenye kupendeza. Bila ya kufanya hivyo utaonekana sio mwanamke wa kileo.
Lakini leo hii mimi kama wanasayansi wengi duniani kwa kutambua viambato vilivyopo kwenye rangi nyingi za kucha, nimependa kukujuza zaidi na zaidi athari hizo zitokanazo na kemikali hizo. Viambato hivyo vya kemikali ambavyo vina misombo (compounds) inayoweza kusababisha kansa kama vile formaldehyde mpaka zile zinazosambaratisha homoni.
Tafiti mbalimbali zimeweza kugundua Toluene, formaldehyde na dibutyl phthalate –zinazotambulika kwa jina la ‘toxic trio’ kuwa husababisha madhara makubwa ya kiafya kwa wafanyakazi wa saluni nyingi zikiwa ni saluni za kike.
  • Toluene – hutumika kufanya kucha zako kuonekana laini na kufanya rangi isijitenge na kemikali zingine kwenye chupa ya kuhifadhia. Lakini husababisha madhara ya mfumo wa fahamu na uzazi.
  • Formaldehyde -husababisha kansa hutumika kwenye kufanya rangi inate kwenye ukucha na kama disinfectant kwenye vifaa vinavyotumika wakati wa upakaji wa rangi za kucha.
  • Dibutyl phthalate husaidia kung’arisha kucha yako lakini inaweza kukusababishia matatizo ya uzazi

Vyumba vingi vya saluni vinakosa madirisha ya kutosha kuwezesha hewa iliyopo ndani kutoka kirahisi na iliyopo nje kuingia ndani. Kwa namna hiyo kemikali nyingi zinazotoka kwenye bidhaa hizi za kutengenezea kucha hubaki ndani na kuwafanya wateja na wafanyakazi wa saluni hizi kuendelea kuzungukwa na kemikali hizi kwa muda mrefu.
Kwahiyo kasi ya kupata madhara yatokanayo na kemikali hizi huongezeka. Kwanza kabisa wanapata madhara ya moja kwa moja kutokana na kemikali hizo, pili wanaendelea kuvuta hewa yenye kemikali hizi ndani ya chumba kidogo cha saluni kisicho na mzunguko wa hewa wa kutosha.
Madhara yatokanayo na kemikali hizi yanaweza sababisha muwasho wa ngozi, matatizo ya macho, na aleji (allergic reactions). Pia hupunguza uwezo wa kufikiria, na wakuhifadhi kumbukumbu, kichefuchefu,matatizo ya mfumo wa upumuaji, kansa,ukuaji na matatizo ya uzazi. Na pia mtu anaweza pata madhara ya muda mfupi kama maumivu ya kichwa na upumuaji.
Kemikali hizo pia tunaweza kuzihusisha moja kwa moja na matatizo ya uzazi kama vile kutoka kwa mimba, kujifungua kabla ya wakati, na kujifungua watoto wenye uzito na maumbo madogo na matatizo mbalimbali ya mimba. Watu wengi hasa wafanyakazi wa saluni hupata madhara haya bila ya wao kutambua chanzo chake.
Nitoe wito kwa wamiliki wa saluni kuhakikisha vyumba vya saluni zao vinakuwa na madirisha yenye ukubwa wa kutosha ili kuwezesha kuwa na mzunguko wa hewa wa kutosha kupunguza hatari zinazoweza sababisha matatizo mbalimbali ya kiafya yatokanayo na kemikali hizo.
Your Health, My Concern
IMEANDIKWA NA
FORD A. CHISANZA
Scientist/Researcher
Intern pharmacist
Tanzania Food And Drug Authority (TFDA)
Location: Off Mandela Road, Mabibo – External,
P.o.Box: 77150, Dar Es Salaam, Tanzania.
Mobile:+255 652466430/+255 684363584
Email: fordchisanza@gmail.com
fordchisanza@yahoo.com




Source : TUBONGE TZ
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment