MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imetoa zuio la muda kwa Jeshi la Polisi kuacha kumkamata Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe hadi maombi yake ya kupinga kukamatwa aliyowasilisha mahakamani hapjana yatakaposikilizwa Ijumaa Februari 24, mwaka huu, saa saba mchana.
Aidha mahakama hiyo pia imemtaka Mbowe kurekebisha hati ya mashtaka na kumwingiza Mwanasheria Mkuu wa Serikali, katika kesi yake ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro na Mkuu wa Upelelezi wa kanda hiyo, Camilius Wambura aambapo ametakiwa kuyawasilisha Jumatatu, Februari 26, mwaka huu.
Wakati kesi hiyo ikiendelea katika chemba namba 64, mahakamani hapo, Kamanda Wambura pekee kati ya walalamikiwa waliotajwa katika kesi hiyo ndiye aliyeonekana mahakamani hapo na kupotea ambapo haikufahamika mara moja alikwenda wapi.
Kesi hiyo itasikilizwa tena Machi, 8 mwaka huu. Katika kesi hiyo, Mbowe anasimamiwa na mawakili Peter Kibatala, Tundu Lissu, Albert Msando, na John Mallya.
from Blogger http://ift.tt/2kI1xOC
via IFTTT
0 maoni:
Post a Comment