Mayanja amesema walipoishika Yanga na kushinda wakiwa pungufu


Kocha msaidizi wa Simba Jackson Mayanja amesema haikuwa rahisi kupata ushindi kwenye Dar derby ukizingatia walikuwa pungufu kufatia mchezaji wao Bokungu kutolewa nje kwa kadi nyekundu.

Mayanja amesema fitness waliyokuwanayo wachezaji wao ilisaidia kwa kiasi kikubwa kutoka nyuma na kushinda dhidi ya Yanga.

“Timu kutoka nyuma tukiwa pungufu kwa mchezaji mmoja, inaonesha ni jinsi gani tunautaka ubingwa wa mwaka huu na hicho ndicho tulikuwa tunakitaka. Tulisema tangu mwanzo ushindi ni lazima hakuna sare, nawapongeza wachezaji wetu.”

“Fitness ya wachezaji wetu ilikuwa juu sana kuliko ya Yanga nafikiri ndio moja ya siri ya kutoka chini na kuweza kushinda tukiwa pungufu. Simba mwaka huu hatutegemei mchezaji mmoja ndio maana kila mara tunabadilisha wachezaji kulingana na mechi na kila mchezaji anaeingia anaweza kufanya kazi.”

“Maandalizi yalikuwa mazuri hasa kwenye upande wa fitness nafikiri ilikuwa ni nzuri kwa uapande wa timu yetu ndio maana tuliweza kutoka nyuma na kushinda mechi, kwa derby ni moja katika ‘come back’ kali kuwahi kutokea.”

“Ilikuwa ni mechi ya kiufundi, hata kabla ya mechi tulitaka sana kushinda. Yanga ni timu nnzuri sana inacheza mechi za kimataifa na wanauzoefu, lakini kwakuwa tuliweza kushinda mechi zingine lazima tushinde ili tuweze kuwa mabingwa na kama Yanga wangeshinda leo ingejiweka vizuri pale juu.”

Kuhusu mwamuzi wa mchezo wao dhidi ya Yanga Mayanja amsema: “Nadhani waamuzi walifanya kazi amekosea hapa na pale lakini amefanya kazi nzuri lakini siwezi kuongelea sana kuhusu hilo kwa sababu mimi sijasomea uamuzi.”
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment