AUDIO: Sababu za Yanga kupoteana mbele ya ‘Mnyama’


Waswahili wnasema kila kitu hutokea kwa sababu, Kocha msaidizi wa Yanga Juma Mwambusi ametoa sababu za kipigo cha Yanga kutoka kwa mahasimu wao Simba SC.

“Baada ya kuanza vizuri, tulipata goli la kuongoza lakini umakini ulipungua kwa wachezaji wetu wakaona game iko kwetu kwa sababu tunaongoza lakini Simba walicheza vizuri katikati kwa kuongeza namba lakini sisi tulikuwa tunachelewa sana, wachezaji waliopewa majukumu ya kuongeza namba walikuwa wanachelewa kutima majukuma yao.”

“Tulikuwa na nafasi kama mbili za kuongeza magoli kipindi cha kwanza lakini umaliziaji ulikuwa hafifu tukaondoka kipindi cha kwanza bila kupata goli la ziada lakini wenzetu baada ya kutoka mtu mmoja wakapata ushindi.”

“Mara nyingi timu ikiwa na upungufu wa mtu wachezaji wanajitoa na kuona hawana cha kupoteza ukizingatiz wamefungwa kwahiyo wakaamua kuja kwa kila kitu.”

“Tumeshafungwa akili yetu tunaielekeza mbele ya safari, Simba walishatutangulia kwa point inane lakini tukawafikia. Bado kuna mechi lolote linaweza kutokea, lengo letu halijafa kwa kupoteza mcheo dhidi ya Simba kupoteza mechi moja hainamaana tumeshapoteza ubingwa tunajipanga kwa mechi zijazo.”

Previous articleAUDIO: Mayanja amesema walipoishika Yanga na kushinda wakiwa pungufu
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment