China imetangaza kuunga mkono Kiongozi Mkuu wa Hong Kong, C Y Leung, anapokabiliwa na maandamano makubwa ambayo yamedumaza shughuli katika eneo kubwa la mji huo.
Wanafunzi wametisha kuanza kupiga kambi baadhi ya majengo ya Serikali iwapo kiongozi huyo hatajiuzulu ifikapo leo jioni.Katika tahariri ya ukurasa wa mbele katika gazeti la kila siku la Kikomunisti Serikali inamuunga mkono kikamilifu na inamwamini na kuridhika na kazi yake.
Wandamanaji wanaendelea kushinda na kukesha katika maeneo muhimu hapo jijini kama vile pande mbili za bandari ya Hong Kong, kama hatua ya kuitisha Demokrasia zaidi.
Serikali ya China imemuunga mkono bwana Leung kwa vile alivyokabiliana na hali Hong Kong na pia kup[ongeza polisi kwa namna wanavyokabili maandamano ya maelfu ya watu mjini humo.
Wengi wamekerwa na tamko la China kuwa lazima wanasiasa wenye nia ya kuwania nafasi mjini Hong Kong lazima wakaguliwe na serikali ya China kwa sababu ya uchaguzi utakaofanyika mwaka 2017.
Serikali imetyaka waandamanaji hao kusitisha maandamano yao ikilaani ghasia na vurugu
0 maoni:
Post a Comment