Mchezaji wa Barcelona Neymar na klabu yake wanakabiliwa na mashtaka ya ufisadi kuhusiana na uhamisho wake kutoka timu ya Santos ya Brazil, baada ya rufaa yake kupingwa.
Kesi hiyo itokana na malalamiko kutoka kwa kundi la uwekezaji la Brazil DIS, ambalo lilimiliki asilimia 40 ya haki za uhamisho wa Neymar.
Kundi hilo linadai kupokea pesa kidogo kinyume na matarajio yao wakati Neymar alipojiunga na Barca kutoka Santos kwa kitita cha pauni milioni 49 mwaka 2013.
“Klabu ya Santos FC, mamake Neymar Nadine Goncalves, na kampuni ya familia ya N&N inayomilikiwa na wazazi wa mchezaji huyo mweye umri wa miaka 25 pia watakabiliwa na mashtaka ya ufisadi na kutumia udanganyifu,” Mahakama kuu ya Uhispania imesema katika taarifa yake.
Waendesha mashtaka wanataka mchezaji huyo kufungwa kwa miaka miwili na kutozwa faini ya karibu pauni milioni 8 .
Hata kama mchezaji huyo wa kimataifa atapatikana na hatia, itakuwa vigumi kwake kufugwa jela.
Barca walidhani wamemaliza kesi hiyo, wakati jaji alipofunga kesi hiyo mwezi Juni mwaka jana, lakini mwendesha mashtaka wa umma wa Uhispania alifanikiwa kuifufua kesi hiyo mwezi Septemba na kusababisha kesi hiyo kuendelea.
Mchezaji mwenza wa Neymar, Lionel Messi alihukumia kifungo cha miezi 21 kwa udanganyifu wa ushuru mwezi Julai mwaka jana.
from Blogger http://ift.tt/2lIsJMH
via IFTTT
0 maoni:
Post a Comment