VITUO VINNE IKIWEPO CLOUDS FM VYATOZWA FAINI, TCRA YAFAFANUA MAKOSA YAO

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imevitoza faini na kuvipa onyo kali vituo vinne vya utangazaji kwa kosa la kukiuka msharti ya utangazaji.
Licha ya kutozwa faini ya TZS milioni 12, vituo hivyo vimetakiwa kuomba radhi kwa siku tatu kwa kusoma maandandiko yatakayoandaliwa na TCRA.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA, Valerie Msoka alisema kuwa vituo hivyo ni Clouds Fm, Star Tv, Times Fm na Channel ten ambapo kila kimoja kimetozwa faini ya TZS milioni 3. Kiongozi huyo alifafanua kosa la kila kituo kuwa ni;
Kwa upande wa Star Tv, Oktoba 13 mwaka jana, ilirusha kipindi cha maigizo cha Futuhi kulichorusha maudhui ambayo yanajenga chuki kati ya Walimu na Wanafunzi. Igizo hilo lilionyesha wanafunzi wakitumia silaha za jadi kumshambulia mwalimu wa darasa.
Pia, Clouds Fm imetozwa faini ya TZS milioni 3 kufuatia mtangazaji mmoja wa kipindi cha Jahazi kuigiza sauti ya mchungaji mmoja akimlaghai mwanafunzi ili afanye naye mapenzi. Alisema kuwa mtangazaji huyo alisikika akisema “njoo nikuhudumie bwana” kwa kutumia sauti ya mchungaji huyo kitu ambacho kinakiuka maadili ya utangazaji.
Kituo cha tatu kutozwa faini na kutakiwa kuomba radhi ni kituo cha Channel Ten, ambapo kimekiuka maadili ya utangazaji baada ya mmoja wa watangazaji wake Novemba 11 mwaka jana kutaja jina la mwanamke ambaye mtoto wake alilawitiwa na dereva wa bodaboda maeneo ya Buguruni, Dar es Salaam.
Mbali na kutaja jina, mtangazaji huyo alitaja eneo muathirika huyo anapoishi kitu ambacho kinaweza kusababisha fedheha kwa mtoto huyo.
Times Fm nao pia wametozwa faini ya TZS milioni 3 na kutakiwa kuomba radhi baada ya kurusha kipindi cha Twenzetu Oktoba 11 mwaka jana ambapo walimhoji mwanamke mmoja ambaye alikiri kuwa alikuwa akitembea na shemeji yake kwa lengo la kujiongezea kipato.
Mwanamke huyo alikiri kuwa na uhusiano wa kimapenzi na shemeji yake ambapo pia watangazaji walimhoji shemeji huyo aliyetajwa na mwanamke huyo. Wakati kipindi hiki kikirushwa, hata watoto walikuwa wakisikiliza redio kitu ambacho kinapelekea uvnjifu wa maadili.
Aidha, Msoka lisema kuwa, kituo chochote chenye leseni ya utangazaji kinatakiwa kuzingatia maudhui ya utangazaji ikiwa ni pamoja na kufikisha ujumbe sahihi kwa jamii.

from Blogger http://ift.tt/2moKtdu
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment