Alichozungumza Ruge kwenye robo fainali ya Ndondo Cup Keko vs Stimtosha

Mkurugenzi wa vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba alikuwa ni miongoni mwa wadau waliohudhuria mchezo wa robo fainali ya Ndondo Cup kati ya Keko Furniture dhidi ya Stimtosha zilizokuwa zikipambana kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.
Wakati wa mapumziko, Ruge alipata fursa ya kuzungumzia michuano hiyo wakati akihojiwa na Azam TV. Alinzungumzia mambo mengi ikiwemo kuhusu kuipelekea Ndongo mikoani pamoja na changamoto za soka la Tanzania.
“Nimevutiwa na mandhari, nilikuwa naona kwenye TV lakini leo nimekuja, namna ambavyo kuna amani kuna amshaamsha kubwa na mpira mzuri sana.”
“Kwa mwamko uliopo wa kuja kuangalia vipaji vinavyotoka chini, naona kabisa timu mpya ya Tanzania inatengenezwa halafu kitu kikibwa ninachojifunza kwenye Ndondo ni ushirikiano, hapa kuna Azam TV, pale kuna Clouds, chama cha mpira Dar es Salaa, chama cha mpira Kinondoni, kuna wadau wengi wanapigania kitu kimoja kupata talanta bora na mabadiliko makubwa kwa ajili ya mpira wetu.”
“Mashindano ya Ndondo yanaelekea Dodoma pia, leo nimetoka kuongea na Mh. Mavunde wa Dodoma nimepata maombi kutoka kwa Lusinde wote wanataka Ndondo iende Dodoma. nadhani kipindi cha Bunge tutakuwa tunaenda Dodoma kuanza Ndondo. Kwa muamko tunaopata nadhani kitakuwa kitu kikubwa sana.”
“Malengo yetu ni kuufanya mpira uwe biashara halisi, watu waelewe kwamba tunaposema mpira pesa sio pesa sio kutoka kwa wadhamini, watu wajenge vipaji ambavyo vitakuwa brand mpya kutengeneza wadhamini wadogowadogo watakaoweza kudhamini kutoka kwenye level ndogo za ligi. Tusiangalie udhamini mkubwa tu wa ligi kuu udhamini ukianza kwenye level ndogo ndio tunakuza thamani ya mpira wetu.”
“Tatizo la tanzania ni vijana wenye vipaji kukosa mwendelezo, unaona vijana wazuri lakini wanapotoka U17 nani anawaangalia kwenda U20 wanapotoka hapo nani anawaangalia kwenda U23, kukosekana kwa huu mtiririko ndio unasababisha wachezaji wanapotea.”
Michuano ya Ndondo imeendelea kuwakutanisha watu mbalimbali wa maeneo tofauti kushuhudia vipaji vya vijana wengi ambao hawana majina wanaoongozwa na wachache wenye majina waliowahi na wanaocheza kwenye vilabu vya ligi kuu lengo ikiwa ni kuwajengea mwamko wa kufika mbali zaidi.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment