Katika ugonvi kati ya Umoja wa Ulaya na
Urusi,serikali mjini Moscow inasemekana imeandaa
orodha ya majina ya wanasiasa wa Umoja wa Ulaya
ambao hawataruhusiwa kuingia nchini humo.Hayo
amearifiwa na ubalozi wa Ujerumani mjini
Moscow,amesema mwenyekiti wa kundi la wabunge
wa chama cha walinzi wa mazingira katika bunge la
Ulaya,Rebecca Harms mjini Brussels.Mwanasiasa
huyo wa chama cha walinzi wa mazingira cha
Ujerumani alikuwa katika uwanja wa ndege wa
Moscow jana na kukataliwa ruhusa ya kuingia nchini
humo.Alikuwa aende Moscow kusikiliza kesi dhidi ya
rubani mmoja wa helikopta wa Ukraine.Sababu
mojawapo aliyopewa ya kukataliwa kuingia Urusi ni
kwamba ameunga mkono vikwazo vya Umoja wa
Ulaya dhidi ya Urusi, anasema mwanasiasa
huyo.Uamuzi wa Urusi wa kumkatalia ruhusa
mbunge Rebecca Harms umewakasirisha wengi
miongoni mwa wakuu wa Umoja wa Ulaya.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 maoni:
Post a Comment