Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum akitoa hotuba ya uzinduzi wa Bodi Mpya ya PPF na Mafao Mapya ya Mfuko huo Dar es Salaam jana.
Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum, (kushoto), akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh. milioni moja, mwanachama wa mfuko huo, Sara Haule kama malipo ya fao la uzazi katika hafla ya uzinduzi wa bodi hiyo sanjari na uzinduzi wa fao la uzazi.
Waziri Fedha, Saada Mkuya akipeana mkono wa pongezi Mwanachama wa mfuko huo, Caroline Kiswaga, baada ya kumkabidhi sh. milioni moja ikiwa ni malipo ya fao la uzazi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Ramadhan Khijjah (kushoto), akimkabidhi kadi ya kujiunga na huduma mpya za mfuko huo, Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum, wakati wa hafla ya uzinduzi wa bodi mpya ya wadhamini wa mfuko huo Dar es Salaam jana. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio.
Wajumbe wa Bodi ya PPF ndani ya uzinduzi.
Meneja Uhusiano wa PPF, Lulu Mengele, akishangilia katika uzinduzi huo wakati Waziri Saada Mkuya alipokuwa akiwapongeza Mfuko huo kupata tuzo ya hesabu bora.
Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio, akizungumza katika uzinduzi huo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Ramadhan Khijjah, akitoa hutuba yake katika uzinduzi huo.
Meneja Kiongozi Mratibu wa PPF, Mbaruku Magawa, akielezea kuhusu fao la uzazi. |
Waziri Saada Mkuya (katikati), na viongozi wengine wakipiga makofi wakati wa uzinduzi huo.
Uzinduzi ukiendelea.
Waziri Saada Mkuya Salum, Mwenyekiti wa Bodi ya PPF, Ramadhan Kijjah, na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, William Erio, wakiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa bodi ya PPF.
Waziri wa Fedha, Saada Mkuya, akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi ya PPF na wakina mama waliopata malipo ya fao la uzazi.
Na Dotto Mwaibale
BODI ya Uhasibu NBAA imeipatia tuzo ya hesabu bora Mfuko wa Pensheni wa PPF yenye thamani ya zaidi ya sh.trilioni 2 kutokana kuwa na hesabu bora kati ya taasisi 40 za Serikali na Mashirika ya Umma.
Hayo yalielezwa na Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum wakati wa uzinduzi wa bodi mpya ya wadhamini wa mfuko huo na Mafao mapya ya mfuko wa Pensheni wa PPF Dar es Salaam jana.
“Nemefurahishwa kwa tuzo hiyo mliyopata hii inaonesha kiashiria cha utendaji uliojaa uadilifu jambo ambalo bila shaka linatoa faraja kubwa kwa wanachama na kuwapa uhakika wa kupata pensheni zao wakati utakapowadia” alisema Salum.
Salum alisema hatua hiyo ya mafanikio ya mfuko huo imethibitisha kuwa taasisi za umma zinaweza kufanya kazi kiasi cha kuwa mfano wa kuigwa kinyume cha dhana potofu iliyopo katika jamii kuwa Serikalini na katika mashirika na taasisi za umma kumejaa ubabaishaji.
Alisema tija na tuzo za kimataifa ilizopata mfuko huo sio tu vinafaida kwa mfuko na wanachama bali pia kwa uchumi wa nchi ya Tanzania na na ni fahari kwa nchi katika medani ya kimataifa.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa mfukio huo, Ramadhan Khijjah alisema thamani ya mfuko huo imeongezeka kwa zaidi ya sh.trilioni moja ndani ya miaka mitatu kutoka sh. bilioni 859.5 mwezi Septemba 2011 hadi kufikia sh.trilioni 2.1 mwezi Juni mwaka huu.
Alisema mfuko huo umeweza kupata mapato yatokanayo na uwekezaji ya jumla ya sh. bilioni 318 mwaka 2013 na sh. 496.5 bilioni mwaka 2014/ 2015 ambapo ni sawa na asilimia 22 na 26.
Alisema hali hiyo imejidhihirisha kuwa mfuko umefanya uwekezaji wenye tija kwa kuzingatia kuwa mfumuko wa bei katika kipindi hicho ulikuwa na wastani wa asilimia 7.9 na 5.7.
from Blogger http://ift.tt/1U6Iusm
via IFTTT
0 maoni:
Post a Comment