PICHA: WAJUE VIONGOZI KUMI WA NCHI WENYE UTAJIRI MKUBWA ZAIDI DUNIANI

Ifuatayo ni orodha ya viongozi kumi wa nchi wenye utajiri mkubwa zaidi duniani.
10. Albert II, mtoto wa Malkia Grace wa Monaco
Ni mtoto wa Malkia Grace, ana asili ya Marekani. Kwa sasa anamiliki kisiwa cha Monaco, utajiri wake ni dola za Marekani bilioni 1 – sawa na shilingi trilioni 2.24.
9. Nursultan Nazarbayev , Rais wa Kazakhstan
Amekuwa madarakani tangu kuanguka kwa ujamaa chini ya Umoja wa Sovieti na amekuwa akishutumiwa sana kwa rushwa na ubadhirifu. Ana utajiri wa dola za Marekani bilioni 1.3 sawa na shilingi trilioni 2.92
8. Mohammed VI, Mfalme wa Morocco
Ni mmoja wa wafanyabiashara wakubwa sana nchini Morocco na hana tuhuma zozote zinazomhusisha na ubadhirifu wa mali za umma. Kwa sasa ana utajiri wa dola za Marekani bilioni 2.5 ambazo ni sawa na shilingi trilioni 5.6
7. Donald Trump, Rais wa Marekani
Donald John Trump ni mfanyabiashara, mwendesha kipindi cha televisheni, mwanasiasa na Rais wa 45 wa Marekani tangu Januari 20 mwaka huu.
6. Hans Adams, Mtoto wa Mfalme wa Liechtenstein
Anamiliki mabenki na kazi mbalimbali za sanaa. Ingawa anasema kuwa demokrasia ndio mfumo bora zaidi wa utawala, uwepo wake katika familia ya kifalme unafanya maneno yake yapuuzwe. Utajiri wake unakadiriwa kuwa dola za Marekani bilioni 4, sawa na shilingi trilioni 8.96.
5. Mohammed bin Rashid Al Maktoum, Waziri Mkuu wa Umoja wa Falme za Kiarabu
Ameibadilisha Dubai kuwa na muonekano mpya kabisa wa kisasa na anamiliki asilimia 99.6% ya kampuni zinazomiliki majengo yote nchini Dubai. Utajiri wake ni dola za Marekani bilioni 18, sawa na shilingi trilioni 40.32 ambazo zinamfanya awe miongoni mwa viongozi matajiri zaidi duniani.
4. Hassanal Bolkiah, Sultani wa Brunei
Anamiliki eneo binafsi kubwa zaidi nchini Brunei na huwa anarusha mwenyewe ndege yake kubwa aina ya Boeing 747-400. Anamiliki magari mengi sana ya kifahari kwa ajili ya matumizi yake tu. Ana utajiri wa dola za Marekani bilioni 20, sawa na shilingi trilioni 44.8
3. Salman bin Abdulaziz Al-Saud, Mfalme wa Saudi Arabia
Baada ya aliyekuwa kaka yake kufariki, Salman akawa Mfalme, akiwa na umri wa miaka 80. Pesa zake nyingi zinatokana na biashara ya mafuta na kwa sasa ana utajiri wa dola za Marekani bilioni 21, sawa na shilingi trilioni 47.
2. Khalifa bin Zayed al Nahyan, Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu
Anakumbukwa sana kwa mchango mkubwa aliowahi kutoa wa dola milioni 460 (sawa na shilingi bilioni 103). Japokuwa anaishi maisha ya anasa za kupindukia, utajiri wake bado ni mkubwa – ambao kwa sasa ni dola za Marekani bilioni 23, sawa na shilingi trilioni 51.5
1. Bhumibol Adulyadej, Mfalme wa Thailand
Ni kiongozi tajiri zaidi duniani, mwenye sifa kubwa sana nchini mwake na utajiri wa dola za Marekani bilioni 30 sawa na shilingi trilioni 67.2.

from Blogger http://ift.tt/2kh995o
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment