UTAJIRI WA MAKONDA WAZUA UTATA

Mbunge wa Geita vijijini, Joseph Musukuma amesema Bungeni kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mh. Paul Makonda anastahili kuchunguzwa kutokana na mali nyingi anazomiliki sasa ndani ya kipindi kifupi ikiwamo jengo la ghorofa, viwanja na magari ya kifahari.
Mbunge huyo alisema kuwa mwaka 2015, Makonda hakuwa na utajiri alionao sasa, hivyo ametaka achunguzwe ni kwa namna gani amebadilika ghafla baada ya kushika nafasi za ukuu wa Wilaya na baadae ukuu wa Mkoa, huku akisisitiza kuwa yeye yuko tayari kuvisaidia vyombo vya dola kuonesha utajiri aliojilimbikizia mkuu huyo ndani ya kipindi kifupi.
Alitaja sababu nyengine za kumchunguza Makonda kuwa ni pamoja na kufanyia ukarabati ofisi yake kwa shilingi milioni 400, na pia akayataja magari ya kifahari anayomiliki katika kipindi hicho kifupi kuwa ni pamoja Lexus alilosema lina thamani ya shilingi milioni 400 na jingine aina ya V8.
“Anatumia Lexus ya petrol ya shilingi milioni 400, lakini imekarabatiwa ofisi ya RC Dar es salaam kwa zaidi ya shilingi milioni 400 bila kufuata utaratibu wa ununuzi wa serikali. Ana ma-V8 na Mwanza amejenga jengo la ghorofa…na hawa Mawaziri tulionao humu kwa nini wamepigwa ganzi? Utawala Bora, Mambo ya Ndani na Waziri wa Sheria, kwanini wamepigwa ganzi?” alihoji.
“Tunataka RC Makonda achunguzwe mali alizonazo…kwa mwaka mmoja huwezi kumiliki magari ya kifahari, ukajenga Mwanza, ukaenda Marekani, ukanunua maviwanja. Wala sio suala la kuogopa. Mimi nasema nipo tayari kuwasaidia Mawaziri na vyombo vya usalama tuwaoneshe,” alisema.

from Blogger http://ift.tt/2kpxBCx
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment