ZIJUE NJIA KUU 5 ZA UINGIZWAJI MADAWA YA KULEVYA NCHINI

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam amesema kuwa utafiti unaonesha kuwa katika sehemu ambazo ni rahisi kuingiza dawa za kulevya duniani kote ni Dar es salaam inaongoza. Miongoni mwa njia ambazo wafanyabiashara wanazitumia ni meli za mizigo ambazo husafirisha dawa kwa kutumia mapipa ambayo huingizwa kwenye meli kwa kutumia boti.

Paul Makonda alitaja njia hizo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu awamu ya pili ya vita dhidi ya dawa za kulevya, ambapo alisoma majina ya watu 65 wanaotakiwa kuripoti Ijumaa kituo cha polisi kati jijini Dar es salaam kwa mahojiano juu ya tuhuma dhidi yao.

Ametaja njia hizi tano zinazotumika kuingiza dawa hizi nchini:


1.Kutumia meli za mizigo

“Watu wanaonunua dawa za kulevya Pakistan wakati meli inapakia mizigo, wao wakitumia boti wanachukua dawa za kulevya na kuzipanga kwenye mifuko kama ile ya sukari. Wanaiweka kwenye mapipa, kuyafunga mapipa hayo na kuyaingiza kwenye meli. Meli ikikaribia huku kwetu, yapo maeneo matatu wanayatumia kutupa mapipa hayo ambayo ni Zanzibar, Bagamoyo na Tanga. Wanayatupa baharini mapipa hayo huku wakiwa wameyafunga GPS (vifaa vyenye teknolojia inayowezesha kuonesha sehemu yalipo) kisha meli inakwenda bandarini kushusha mzigo wake wa halali kama kawaida.


2.Kutumia uagizaji wa magari

Alisema kuwa wafanya biashara hao kuwa ni uingizwaji wa magari. Alisema wafanyabiashara ambao huenda nje ya nchi kununua magari kwa ajili ya kuuza wamekuwa wakitumia fursa hiyo kubeba dawa za kulevya.

“Mtu ananunua magari Japan lakini badala ya kuyaleta moja kwa moja Tanzania anaamua kutumia njia ndefu zaiadi, analipitishia Bombay au Pakistan. Wanaliwekea madawa yao kisha wanalileta nchini.”


3.Sehemu nyengine ni Marekani

“Upo mchezo wa kufungua baadhi ya sehemu za magari na kuingiza dawa za kulevya. Ukichunguza Dar es salaam wapo wenye maghala ya magari na wanaouza kwa bei ya chini, lakini sijasema kuwa kila mwenye ghala la magari anayeuza kwa bei nafuu basi anauza dawa za kulevya.”

4.Kutumia meli za mafuta

“Kazi yetu ni kuangalia kiwango cha mafuta na vitu vinavyozingatiwa, kwa hiyo wanatumia udhaifu huo kufanya yao.” Hivyo Makonda amesema amefanya mazungumzo na mamlaka husika ili waongeze udhibiti uingizwaji wa dawa za kulevya kupitia njia hiyo.

5.Kutumia boti binafsi (yacht)

Watu kuwa na maegesho ya boti zao binafsi, wanachukua mizigo ya dawa za kulevya, kuuingiza kwenye maegesho haya na kupakua mzigo kabla ya kuusafirisha. Kuhusu kukabiliana na hili Paul Makonda amehitaji mmiliki wa Klabu ya Wamiliki wa Boti Binafsi jijini Dar es salaam (Dar yacht club) afike polisi kwa ajili ya mahojiano.

from Blogger http://ift.tt/2kSZx55
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment