WHO yasema Ebola imegundulika Kaskazini Mashariki mwa DRC

media Daktari anayeshughulikia ugonjwa wa Ebola katika shughuli zake za kitabibu Afrika Magharibi mwaka 2013
 
Mlipuko wa ugonjwa hatari wa Ebola umetangazwa Kaskazini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Shirika la afya duniani WHO limethibitisha kutokea kwa mlipuko huo ambao umesababisha vifo vya watu watatu tangu mwaka tarehe 22 mwezi Aprili mwaka huu.
Eneo la msitu wa Equitorial katika mkoa wa Bas-Uele mpakani na Jamhuri ya Afrika ya Kati ndilo lililoathiriwa.
Waziri wa afya nchini humo Oly Ilunga amethibitisha uwepo wa ugonjwa huo lakini akatoa wito kwa wananchi kutokuwa na wasiwasi.
WHO inasema inashirikiana kwa karibu na serikali ya DRC kuhakikisha kuwa wanafanikiwa kudhibiti ugonjwa huo.
Mara ya mwisho kwa Ebola kulikumba taifa hilo, ilikuwa ni mwaka 2014 na kusababisha watu 49 kupoteza maisha lakini baadaye maafisa wa afya wakafanikiwa kuudhibiti.
Ugonjwa huu ulisumbua sana Mataifa ya Magharibi mwaka 2013 na kusababisha vifo vya watu 11,300 na kuwambukiza wengine nchini Guinea, Sierra Leone na Liberia.
 


 
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment