Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu
Tanzania Bara, Young Africans wametoka vifua mbele baada ya kuwachapa
mabao 2-0 wapinzani wao Tanzania Prisons katika mchezo uliochezwa uwanja
wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Mabao
hayo yote mawili yamepatikana katika dakika 45 za kipindi cha pili cha
mchezo huo ambapo ilipofika dakika 71 Amisi Tambwe aliweza kuchungulia
nyavu za wapinzani wao kwa mara ya kwanza na kuifanya Yanga kuongoza bao
1-0 na ilipofikia dakika 76 za mchezo Obrey Chirwa aliwainua tena
mashabiki wa klabu hiyo kwa kufunga bao la pili na kuifanya timu yake
kuibuka kidedea mpaka mpira kuisha.
Kwa matokeo hayo timu ya Yanga imeweza kujiongezea pointi zake 3 na kuifanya kufikia alama 59 sawa sawa na Simba SC.
Katika hatua nyingine Nahodha wa
Prisons, Benjamini Asukile amesema pamoja na kufungwa na Yanga bado
hawajakata tamaa na Prisons lazima itabaki Ligi Kuu Bara.
“Kuna makosa tulifanya
kipindi cha pili na Yanga wakaitumia nafasi hiyo. Lakini tutaendelea
kupambana na imani yetu Prisons itabaki ligi kuu". Alisema Asukile
0 maoni:
Post a Comment