Msanii wa filamu Shamsa Ford
amefunguka na kumtetea Flora aliyewahi kuwa mke wa Emmanuel Mbasha
ambaye wiki iliyopita aliolewa tena na kijana Daudi Kusekwa
Shamsa
Ford ameibuka na kuanza kumtetea Flora kutokana na maamuzi yake hayo ya
kuolewa kwa mara ya pili na kusema yeye ndiye anajua kwanini ameamua
kufanya hivyo na kumtaka kutosikiliza maneno ya watu.
"kwanza kabisaa ningependa
kukupongeza kwa kuolewa dada yangu hakika mlipendeza sana. Dada yangu
nina uhakika umekutana na mitihani mingi sana kwenye maisha yako na
ukaweza kupambana nayo. Basi hata haya wanayoongea binadamu ona kama
wanaimba mziki tu..Binadamu siku zote ni waongeaji hata uwafanyie nini
hawawezi kuacha kuongea. Wewe ndiyo unayejua umuhimu na upendo wa mumeo
basi inatosha. Hakuna binadamu anayepasa kumuhukumu binadamu mwenzie
zaidi ya Mwenyezi Mungu pekee yake. Fanya unachoona ni sahihi kwako wewe
na Mungu wako tu" alisema Shamsa Ford
Shamsa aliendelea kusisitiza
"Hizi kelele za binadamu
zisikunyime raha wala amani dada yangu awe kijana, awe mzee, awe mdogo,
awe masikini, awe tajiri, awe mbaya, awe mzuri yote haijalishi kwa
sababu ni wa kwako na wala hujamuomba mtu akusaidie kukaa na
mumeo...Inshaallah Mwenyezi Mungu aibariki ndoa yenu iwe ya furaha na
amani" alisema Shamsa Ford
0 maoni:
Post a Comment