Mchekeshaji Steve Nyerere
ameendelea kufunguka mambo mengine mapya kwa kudai kinachosababisha kufa
kwa filamu za bongo ni wasanii wenyewe kushindwa kutambua ushidani wa
kibiashara katika soko ukoje.
Mchekeshaji Steve Nyerere
Steve
amebainisha hayo kupitia kipindi cha eNewz huku akisema adhani kama
wanapaswa kuendelea kushindana na wamachinga wanaosambaza na kuuza 'CD'
katika soko la Karikakoo kwa kuwa wao wanachokiuza ni kile ambacho
kinauzika kwa jamii nasiyo vinginevyo.
“Sidhani kosa letu ni hawa
wamachinga, machinga wanauza ‘Product’ ambayo inauzika nje. Filamu moja
ya kizungu ambayo ina ‘part 1’ ni shilingi elfu mbili na mia tano
(2,500), wewe ‘Part 1 &2’ unauza shilingi elfu sita (6,000) kwa hali
gani ya maisha ?”. Alisema Steve
Katika hatua nyingine, Steve aliendelea
kurusha lawama zake kwa wasanii kwa kudai wao ndiyo chanzo kikubwa cha
kuiangamiza tasnia ya filamu kwa kuwa wengi wao hawapendi kufikilisha
akili zao katika kutengeneza kazi zilizokuwa bora kwa jamii ila
wanachokitazama zaidi ni kupata faida kubwa kwa kazi mbovu.
“Hiyo ndiyo sumu ambayo ipo
na inatufanya mpaka leo hatupo katika umoja, kwanza ili tuweze
kufanikiwa mafanikio hayapo ya mmoja mmoja, mafanikio yote duniani
yalipita kwa watu ndiyo wewe ukafanikiwa kwa hiyo lazima tukubaliane,
tupendane na nyoyo zetu ziwe zimefunguka kwa kufanya vitu vizuri,
tunawaza sana gharama za movie kuliko kufanya kitu kizuri kwa gharama ni
bora upate laki 2 faida lakini ‘site’ iseme huyu mtu ni sahihi”.Alisema Steve
Aidha Steve aliendelea kusisitiza kwamba “Kuna
ma-director wazuri zaidi lakini leo wote hawapo, wanachokikosa ni
ushirikiano, tunao ma-director wazuri tu, wanaweza wakafanya kitu kizuri
tu ‘site’ lakini ushirikiano hawana kuna watu wanakuwa Mungu watu
haiwezekani, haiwezekani kuwa Mungu mtu jamani Mungu ni mmoja tu”- Steve aliendelea kusisitiza
0 maoni:
Post a Comment