UDUGU WA KIISLAMU WAPANGA MAANDAMANO

udugu wa kiislamu wapanga maandamano zaidi
Wakikaidi ukandamizaji unaofanywa na serikali ya mpito inayo ungwa mkono na jeshi,kundi la udugu wa kiislamu na washiriki wao wametangaza kuwa watafanya maandamano katika maeneo karibu tisa katika mji mkuu wa Misri,Cairo.

Waandamanaji watakusanyika karibu na mahakama ya katiba kusini mwa mji wa Cairo

Waungaji mkono wa Rais aliye ondolewa madarakani mohamed Mursi wanapanga kufanya maandamano mengine mjini Cairo leo jumapili (18.8.2013) na kuongeza hofu ya umwagikaji zaidi wa damu baada ya mamia ya watu kuuwawa wki hii.

Kundi la udugu wa kiislamu kufutwa kisheria.


mapambano katika msikiti wa al-fadh 17.8.2013
maandamano hayo yanakuja wakati serikali inatafakari kulivunja kabisa kisheria kundi la udugu wa kiislamu na waendesha mashtaka wanawahoji wafuasi 250 wa mursi kuhusiana na mauwaji na madai ya ugaidi.

\
Hatua ya jeshi kumuondoa madalakani Mursi,julai 3 mwaka huu, baada ya maandamano ya mamilioni ya wamirsi wakidai kujiuzulu,imewagawa kwa kiasi kikubwa wamirsi, ambalo ni taifa lenye wakazi wengi mwiongoni mwa mataifa makubwa.


ndani ya msikiti wa Al-fath mjini cairo 17.8.2013
Shutuma kali
mazishi katika kanisa la captic mjini cairo



Ukandamizaji zidi ya waandamanaji wa makundi ya kiislamu umesababisha shutuma kali kutoka jumuiya ya kimataifa,hususani kutoka bara la ulaya na marekani. Hata hivyo, mataifa ya ghuba yameeleza kuunga mkono watawala wa mpito nchini mirsi.

katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban ki- Moon
Katibu mkuu wa umoja wa mataifa  Ban ki- Moon amesema jana jumamosi 17.08.2013 kuwa anashtushwa na maandamano yenye ghasia pamoja na matumizi ya nguvu kupita  kiasi kwa polisi.





Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment