Mahakama nchini Misri imemuhukumu kiongozi wa Kidini wa Chama
cha Udugu wa Kiislamu, Mohammed Badie na wenziwe saba kifungo
cha maisha kutokana na mashtaka ya kupanga vurugu, kuuwa na
hujuma. Kesi hiyo inatokana na ghasia zilizofanyika msimu wa
kiangazi uliopita baada ya kuondolewa madarakani rais Mohammed
Morsi, ambapo mapigano yaliuwa watu 10 na wengine 20 kujeruhiwa.
Jaji kiongozi katika mahakama, Mohammed Nagi Shehata vilevile
amewahukumu watu sita wenye msimamo mkali wa Kiislamu adhabu
ya kifo pasipokuwepo mahakamani. Kwa mujibu wa sheria za Misri,
kesi yao inaweza kusikilizwa upya pale watakapopanda kizimbani.
Baada ya kuondolewa madarakani rais Morsi, serikali ilianzisha
operesheni yenye lengo la kuwaondosha kabisa waliokuwa
wakimuunga mkono Mursi waliopiga kambi mjini Cairo na kuuwa
mamia ya watu na kuwaweka kizuizini maelfu wengine wakiwemo
maafisa waandamizi wa chama cha Udugu wa Kiislamu.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 maoni:
Post a Comment