Waziri Mkuu wa Lesotho, Tom Thabane amethibitisha kuwa jeshi
limechukua madaraka katika mapinduzi kwenye taifa hilo dogo la
Kifalme na ametorokea taifa jirani la Afrika Kusini kwa kuhofia
usalama wake. Akizungumza na shirika la habari la Uingereza BBC
Thabane amesema ameondolewa madarakani si na watu wa taifa
hilo bali nguvu ya jeshi na kwa hivyo si halali. Aliongeza kusema
amewasili Afrika Kusini leo hii na kwamba atarejea nyumbani haraka
pale atakapo baini maisha yake hayatokuwa hatarini. Waziri mmoja
katika serikali ya taifa hilo alisema jeshi la Lesotho liliweka katika
udhibiti wao makao makuu ya polisi na makazi ya waziri mkuu yaliopo
Maseru kwa masaa kadhaa leo, lakini baadae walijiondoa. Waziri wa
Michezo na Kiongozi wa chama kiitwacho Basotho Natinal Party
Thesele Maseribane amesema jeshi lilikuwa likimtafuta yeye, naibu
waziri mkuu na waziri mkuu wawapeleke kwa mfalme. Jambo hilo
linamaanisha ni mapinduzi katika taifa hilo
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 maoni:
Post a Comment