Kiungo
mshambuliaji mpya wa Manchester United, Angel Di Maria ameandika barua
iliyowasikitisha wachezaji na mashabiki wa Real Madrid.
Di
Maria ambaye ametua Man United kwa dau la pauni milioni 60 ambalo ni
rekodi England, amesema hakupanga kuiacha timu hiyo ya Hispania.
Mashabiki
waliochangia kwenye mtandao wa Twitter wameelezwa kusikitishwa na barua
hiyo huku wakiamini siku moja, Di Maria atarejea tena katika klabu yao.
Amesema
wakati anakwenda kwenye Kombe la dunia baada ya kutwaa ubingwa wa Ulaya
‘La Decima’ akiwa na Madrid, alitarajia kurudi na kuendelea na kazi
yake.
“Hata
hivyo kuna mambo yalijitokeza, yakiwemo ya mshahara wangu na sasa
natarajia kuyapata Manchester United, moja ya klabu kubwa duniani na
nina imani nitaweka historia pale,” alieleza katika sehemu ya barua
hiyo.
Di Maria ameeleza atakavyowakumbuka wachezaji wengi wa Madrid na maisha yao kwa ujumla.
Tayari
Muargentina huyo amemalizana na Man United na baadhi ya wachezaji wa
Madrid kama Cristiano Ronaldo na Sergio Ramos, hawakutaka aondoke.
0 maoni:
Post a Comment