Kamanda wa
polisi wa mkoa wa Ruvuma Mihayo Msekhela
Songea
JESHI la
polisi mkoani Ruvuma linawashikilia askari wake wawili kwa tuhuma za
kumjeruhi kwa kumpiga risasi mwendesha piki piki aliyejulikana kwa jina
la Salgo Ndunguru(22) mkazi wa Ruvuma mjini Songea.
Akizungumza
kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Mihayo Msekhela amesema tukio hilo
limetokea Agosti 26 mwaka huu majira ya saa 12 jioni katika mtaa wa
Mfaranyaki mjini Songea ambapo askari polisi wawili PC Waziri mwenye
namba G 5075 na PC Ayoub mwenye namba G 9800 wakiwa doria na piki piki ya polisi yenye namba za usajili PT 1250 CR aina
ya Yamaha CC 250 katika eneo hilo la Kombezi walimjeruhi mwendesha piki piki
huyo kwa kumpiga risasi.
Amesema
mwendesha piki piki huyo alijeruhiwa kwa kupigwa risasi na askari PC
Waziri katika harakati za kuinsuru silaha hiyo iliyokuwa imebebwa na
askari mwenzake PC Ayoub ambaye
alizingirwa na baadhi ya waendesha piki piki wakiongozwa na mwendesha piki piki
aliyejulikans kwa jina moja la Agrey ambaye alidai kuwa yeye ndiye mmiliki wa
piki piki iliyokamatwa na askari hao ikiwa imebeba mzigo wa majiko.
Ameitaja
piki piki iliyokuwa ikiendeshwa na majeruhi huyo kuwa ni aina ya San Lug
yenye namba za usajili T 757 CUD ambapo baada ya mwendesha piki piki
huyo kukamtwa alimpigia simu mdhamini wake Agrey alipofika alisababisha mkusanyiko mkubwa wa waendesha piki piki maarufu kama Yebo yebo ambao walianza kuwarushia mawe askari hao huku
majeruhi akiwa ameshika mtutu wa bunduki iliyokuwa imebebwa na askari PC Ayoub
ndipo askari PC Waziri katika kuinusuru silaha isiporwe alimpiga risasi
majeruhi kwenye kiganja cha mkono wa kushoto na risasi hiyo kumjeruhi sehemu
mbili ambazo ni kiganja cha mkono wa kushoto na paja la mguu wa kushoto.
Amesema
majeruhi amelazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma iliyopo
mjini Songea kwa matibabu na hali yake inaendelea vizuri na katika
vurugu hizo zilizodumu kwamuda wa nusu saa kabla ya kutulizwa na kikundi cha askari maalumu kilichowahi
na kutuliza vurugu hizo kwa kutumia nguvu kidogo hali ikarejea kuwa shwari na
hakuna madhara zaidi yaliyojitokeza.
Aidha
kamanda Msikhela amesema uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo
unaendelea ili kubaini chanzo halisi cha tukio hilo unaendelea na hatua
zitachukuliwa dhidi ya
wahusika watakaothibitika na ametoa wito kwa waendesha piki piki kuacha tabia
ya kushabikia vurugu ambazo hazina tija na kuwa chanzo cha kusababisha migogoro
isiyokuwa na maana na kusababisha madhara kwa jamii.
Amewataka
waendesha piki piki kufuata taratibu zilizopo ikiwa ni pamoja na
kuwasilisha malalamiko yao kwa viongozi husika kwa kupitia viongozi wao
ili yaweze kufanyiwa kazi amewataka wananchi mkoani Ruvuma kuwa watulivu
na kuendelea na shughuli zao bila hofuyoyote kwani jeshi la polisi liko imara kulinda mali na maisha yao.
0 maoni:
Post a Comment