Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka, 67, amekuwa bosi katika kikosi cha Gunners tangu mwaka 1996 na siku za hivi karibuni amekuwa na wakati mbaya zaidi ndani ya klabu ya Arsenal.
Wenger , alisema hatima yake ndani ya klabu hiyo itaamuliwa na kikao cha Bodi ambacho kitakaa baada ya mchezo wao wa fainali ya FA utakao wakutanisha Arsenal dhidi ya Blues.
Arsene Wenger, atakuwa kocha mwenye mafanikio zaidi kama atashinda kombe la FA Cup kwa kuifunga Chelsea katika mchezo wao wa Fainali.
“Namfahamu sana , Arsene Wenger , amefanya mengi mazuri katika kombe la FA na kushinda mataji ,” alisema Conte.
Conte, anaamini Wenger ataendelea kusalia ndani ya kikosi cha Arsenal akiwa kama meneja katika msimu ujao wa ligi.
“Sitaki kuamini kuwa huu ndio utakuwa mchezo wake wa mwisho ndani ya Arsenal, anastahili kuendelea kuitumikia Arsenal,” alisema Muitaliano huyo ambaye anafikiria kuchukua taji lake la pili katika msimu wake wa kwanza akiwa Stamford Bridge baada ya kuchuku la ligi ya Uingereza.
“Wakati mwingine nafikiria kwa hapa nchini Uingereza unakuwa na thamani kama unapata nafasi ya kushiriki michuano ya klabu bingwa . Ni msimu huu tu ndio haja pata nafasi ya kufuzu kushiriki michuano hiyo, ila amefanya kazi kubwa ndani ya Arsenal”
“Ukiwa umeweza kukaa kwa muda mrefu ndani ya klabu hakika unastahili kuwa meneja bora wa kihistoria na atabaki kuwa hivyo.” alisema kocha wa Chelsea Antonio Conte.
Klabu ya Chelsea haijashinda taji la FA Cup tangu ilipofanya hivyo kwa mara ya mwisho mwaka 2012 wakati wa kocha, Roberto di Matteo na kuifunga Liverpool kwa jumla ya magoli 2 kwa 1 katika dimba la Wembley.
0 maoni:
Post a Comment