Kaimu mwenyekiti wa jukwaa la Katiba Tanzania, Hebron Mwakagenda
akizungumza na wanandishi wa habari leo (hawapo pichani) Agosti 27, 2014
juu ya mwenendo wa bunge la katiba.
Wanandishi wa habari wakimsikiliza, Hebron Mwakagenda kwa makini.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
Wakati mchakato wa katiba Tanzania ukiwa ni kama kitendawili kisicho na majibu sahihi kutokana na mchakato huo kuvurugika na kukosa mwelekeo, nao Jukwaa la Katiba Tanzania (JUKATA) wazidi kumtupia lawama zote za kuvurugika bunge hilo mwenyekiti wa bunge hilo mheshimiwa Samweli Sitta na kudai kuwa ndiye aneyeuvuruga mchakato huo baada ya kugeuza Bunge hilo kama kikao cha Chama cha Mapinduzi (CCM).
Akizungumza na wanahabari muda huu jijini Dar es salaam kaimu mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania Hebron Mwakagenda amesema kuwa JUKATA wamekuwa wakifuatilia mchakato huu wa bunge ka katiba kwa wiki mbili hizi na kubaini mapungufu makubwa sana ambayo yanatokea jambo ambalo linaonyesha wazi kuwa mwenyeikiti wa bunge hilo hana nia wala dhamira ya kulipatia taifa katiba mpya ya watanzania.
Wanahabari mbalimbali wakiwa wanamsikiliza kiongozi huyo wakati wa mkutano Bw Mwakadenga amesema kuwa swala la mahudhurio ya wabunge wanaoshiriki katika kamati mbalimbali za bunge hilo yamekuwa madogo sana na yasiyo ya kuridhisha ikiwa ni pamoja na wabunge wengi kutokuhudhuria katika kamati hizo pamoja na kusaini kulipwa posho za siku jambo ambalo amesema kuwa ni wizi mpya kwa watanzania,
“Kwanza bunge la katiba linaonyesha kuwa wajumbe 441 wamehidhuria lakini uchunguzi wetu unaonyesha kuwa hawa ni wale wote ambao wamewahi kufika na kusaini kwenye kitabu cha mahudhurio wengine wao takribani 100 tuligundua kuwa hawapo bungeni wakiwemo mawaziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na serikali ya mapinduzi Zanzibar pamoja na baadhi ya viongozi wa kamati”amesema Mwakagenda.
Ameongeza kuwa mambo mengine ambayo yanalifanya bunge hilo kuvurugika ni pamoja na kukosekana kwa muafaka na maridhiano ya kitaifa, matumizi mabaya fedha ikiwa ni pamoja na Wajumbe kulipwa bila kuhudhuria bungeni, kukosekana kwa theluthi mbili toka Zanzibar ili kupitisha katiba,pamoja na uondoaji wa vifungu muhimu kwenye rasimu mambo ambayo amesema kuwa mwenyekiti Samweli Sitta ameyafumbia macho na kijifanya kama hayaoni huku akiwa anajua wazi kuwa anauzika mchakato huo.
“Huyu mzee hatujamwelewa kabisa, sisi tumekaa tumezungumza naye tukamuuliza atueleze swala la theluthi mbili hawa wajumbe watapatikana wapi hajatupa jibu la kuridhisha na ukimwona ni kama mtu ambaye ameshachanganyikiwa, anapambana na kila anayekuja mbele yake, iwe mwandishi, mwanaharakati, mbunge, yeye amekaa kujihami tu, sasa hali hii sio nzuri kwa mchakato muhimu kama huu”alisema kiongozi huyo wa JUKATA.
Katika hatua nyingine JUKATA wamemwomba raisi Kikwete kiusimamisha mchakato huu wa katiba hadi kipindi kingine kutokana na kuonekana wazi kuwa hauwezekani na kusema Tanzania imekuwa na michakato mingi ambayo sisi kama taifa hatuwezi kuiendesha kwa wakati mmoja na kupata katiba bora, “Kusema ukweli taifa sasa lina michakati mingi sana mfano mchakato wa vitambulisho vya taifa, uchaguzi wa serikali za mitaa, daftari la kudumu la kupiga kura na michakato mingine mikubwa, hii haitaki usome sana ndo uelewe ni kutumia busara tu kwamba huu mchakato wa katiba hautawezekana tena, sisi tunamwomba mheshimiwa Rais Kikwete awasikilize watanzania na kuusimamisha mchakato huu wa katiba ili tujipange upya kuanza
tena.
Mchakato wa katiba umekuwa ukiendelea jijini Dodoma bila ya mariano na wajumbe waliotoka wa UKAWA huku kukiwa na taarifa kuwa rais amekubali kukutana nao wiki hii kwa ajili ya mazungumzo ya kuunasua mchakato huu.
0 maoni:
Post a Comment