Mpya Nje ya Nchi: Marekani yalaani vita nchini Libya


Mataifa ya magharibi yalaani kuenea kwa vita nchini Libya
Maafisa nchini Marekani wanasema Misri na umoja wa falme za kiarabu zilihusika na mashambulio nchini Libya katika wiki iliyopita kuwalenga wanamgambo wa kiislamu wanaokabiliana na vikosi vya serikali.
Afisa mmoja mkuu wa Marekani ameiambia BBC kwamba Marekani haikushirikishwa katika mashambulio hayo na ilishangazwa.
Makombora hayo yaliofyetuliwa Tripoli yanasemekana kutekelezwa na Umoja wa milki za kiarabu kwa kutumia kambi za kijeshi nchini Misri.
Misiri imekana tuhuma hizo na hapajakuwa na tamko lolote kutoka kwa Umoja wa falme za kiarabu.
Marekani na washirika wake wanne wa Ulaya zimeshutumu wanachokitaja kama usumbufu wa kutoka nje nchini Libya. Ufaransa, Ujerumani, Italia, Uingereza na Marekani zimelaani vikali mpigano na ghasia nchini Libya.
Wapiganaji wa makundi mawili hasimu ndio wanaoendesha mashambulizi hayo
Zimelaani pia kuongezeka kwa mapigano na ghasia ndani na kuzunguka miji ya Tripoli, Benghazi, na nchini kote Libya, hususan dhidi ya maeneo ya maakazi ya watu, sehemu za umma, na miundombinu muhimu kutokana na mashambulio ya ardhini na pia ya angani.
Nchi hizo zimesema zinarudia wito wao, zikiungana na ule wa serikali ya muda ya Libya, Baraza la Wawakilishi na wananchi wa Libya, kwamba pande zote nchini Libya zikubaliane na usitishaji wa vita mara moja na kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kisiasa, kujizuia na mipango inayoweza kudhoofisha hatua hiyo.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment