Serikali ya Syria imesema iko tayari kushirikiana katika juhudi zozote za
kimataifa za kupambana na kundi lenye itikadi kali linalojiita Dola la Kiislamu
nchini humo. Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria, Walid al-Moualem,
amesema leo kuwa yuko tayari kushirikiana na mataifa ya Magharibi
kupambana na Dola la Kiislamu, lakini iwapo mataifa hayo yataheshimu uhuru
wa Syria. Amesema mashambulizi yoyote ya anga yatakayofanywa na
mataifa ya kigeni dhidi ya Dola la Kiislamu nchini Syria, itabidi yaratibiwe
mapema na Syria na bila kufanya hivyo, watayachukulia mashambulizi hayo
kama kitendo cha uchokozi. Hata hivyo, Ujerumani imesema haina mpango
wa kushirikiana na Syria. Wapiganaji wa kundi hilo jana waliidhibiti kambi
muhimu ya jeshi la serikali nchini Syria.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 maoni:
Post a Comment