Afisa Ruzuku kutoka TMF akifungua semina kwa waandishi wa
habari mkoani Mbeya.
Washiriki
wa semina wakiwemo maafisa wa TMF na Wanahabari Mkoa wa Mbeya wakifuatilia kwa
makini
BAADHI
ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mbeya wametoa duku duku lao kwa Mfuko wa vyombo
vya habari nchini(TMF) kuhusu utaratibu wa kupata ruzuku kwa ajili ya kufanya
kazi za uchunguzi.
Malalamiko
hayo yalitolewa jana mbele ya viongozi wa TMF katika semina iliyofanyika katika
ukumbi wa GR Hotel iliyopo Soweto jijini Mbeya ambapo waandishi wa Habari
walipata fursa ya kutoa ya moyoni.
Awali
Afisa Ruzuku wa TMF, Japhet Sanga, katika utangulizi wake aliuliza idadi ya
waandishi waliowahi kunufaika na Mfuko huo kwa Mkoa mzima tangu uanzishwe
ambapo waandishi sita waliweza kujitokeza.
Kutokana
na idadi hizo Afisa huyo alizidi kuhoji ni kwanini idadi iwe ndogo kiasi hicho
ukilinganisha na utitili wa Waandishi wa Habari uliopo Mkoa wa Mbeya.
Wakichangia
hoja baadhi ya waandishi walisema wanahisi kuwepo kwa hali ya upendeleo kwa
baadhi ya waandishi kujirudia kupata ruzuku aidha kwa kuangalia majina ama
kupata chochote kutoka kwa mwandishi(ten percent).
Hata
hivyo changamoto nyingi zilizozungumzwa na Wanahabari, Afisa Ruzuku alisema
zimechukuliwa na kufanyiwa kazi kisha kuendelea na ufafanuzi juu ya namna ya
kuomba ruzuku kwa kufuata vigezo na masharti.
0 maoni:
Post a Comment