Ushabiki ni kitu cha kwanza katika mpira wa miguu,shabiki ni mtu anaye penda "kupita kiasi' kile anachokuwa anashabikia,kama huna sehemu unayoshabikia basi si raisi kupata ladha halisi ya mpira wa miguu katika timu ninayo shabikia ninaweza kuona makosa ya kiufundi kufulaia ushindi ,na vilevile kupata maumivu makali .leo hii ,maisha ya furaha ya mashabiki ya manchester United yapo katika mashaka,ile furaha ya kushangilia ushindi kila mwisho wa wiki si ya kuaminika tena.
Lakini ni hapo shabiki anaweza kuona mapungufu ya timu yake na pengine akajiaminisha kuwa usajili zaidi hauepukiki .kila mtu anaona udhaifu wa United sasa .baada ya kipigo katika uwanja wa Old Trafford kutoka kwa swansea city siku ya ufunguzi United ilisafiri hadi kaskazini magharibi mwa England na kuambulia sare ya kufungana 1-1 na Sundarland katika uwanja wa Stadium of Right.United imefanikiwa kumsaini kiungo mshambulkizi wa kimataifa wa Argentina Angl Di Maria kutoka Real madrid kwa ada ya rekodi England ,pauni milioni 60,Di maria amevunja rekodi ya usajili iliyowekwa na Fernando Torres januari 2011 alipo jiunga na chelsea kwa ada ya pauni milioni 50 kutoka Liver pool.
Kabla ya msimu wa ligi kuu ya England kuaanza United ilikuwa katika kipindi kiziri cha maandalizi nchini Marekani,huko waliweza kupata ushindi zidi ya timu za As Roma ,inter millan,Real madrid ,Liver pool,kabla ya kuishinda Valencia siku chache baada ya kuanza kwa msimu timu ilionekana bora chini ya kocha mpya Luis Van Gaal wachezaji wa safu ya ulinzi Criss Smalling ,John Evance na Phill jones walionekana kuimalika na kucheza vizuri katika mfumo wa 3-5-2 ambao unawapa uhuru wa kushambulia na kukambia katikati ya uwanja walinzi wa pembeni.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 maoni:
Post a Comment