Katibu wa Siasa na uenezi wa CCM Mkoa wa Mbeya, Bashiru Madodi akisoma Tamko hilo.
CHAMA cha Mapinduzi
(CCM) Mkoa Mbeya kimeisimamisha kamati ya siasa Wilaya ya Ileje kwa
utovu wa nidhamu pamoja na kuwasimamisha viongozi wa Chama hicho kata ya
Majengo wilaya ya Momba mkoani Mbeya.
Hayo yalibainishwa
jana na Katibu wa Siasa na uenezi wa CCM Mkoa wa Mbeya, Bashiru Madodi,
alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari ofisi za CCM Mkoa wa Mbeya zilizopo
Sokomatola jijini Mbeya.
Madodi alisema
maamuzi hayo yalifikiwa Agosti 23, mwaka huu baada ya kamati ya siasa ya Mkoa
chini ya Mwenyekiti wake Godfrey Zambi kufanya zxiara ya ghafla katika maeneo
hayo.
Madodi alisema katika
Wilaya ya Ileje chanzo kikubwa cha hali hiyo kutokuwepo kwa maelewano baina ya
Mwenyekiti wa CCM Mkoa na Katibu wake hali iliyopelekea kufunga ofisi kwa muda
wa siku kumi.
Alisema kutokana na
kuwepo kwa mtafaruku huo Kamati iliamua Kuvunja kamati ya Siasa ya Wilaya ya
Ileje, ilipendekeza Vikao vya juu kwa maana kamati kuu ya CCM Taifa imvuee
Uenyekiti Hezron Kibona.
Alisema Kamati pia
imeagiza Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje Mohamed Mwala na katibu
wa Baraza la Madiwani wa CCM kupewa onyo kali na kuwa chini ya uangalizi kwa
muda wa miezi 12 na kutoruhusiwa kuhudhuria vikao vya kamati ya siasa
vinavyotokana na nyadhifa zao.
Pia Katibu Mwenezi wa
CCM Wilaya ya Ileje avuliwe madaraka na wajumbe wote wa kuchaguliwa wa Kamati
ya siasa Wilaya waondolewe moja kwa moja kuwa wajumbe wa kamati ya sioasa ya
Wilaya.
Madodi aliongeza kuwa
Kamati imemuagiza Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Janeth Mbene ambaye pia
ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara kufika katika kikao cha Kamati ya Siasa
ya Mkoa ili kuhojiwa kutokana na kuwa chanzo cha hali hiyo.
Madodi alisema Kamati
Pia ilikutana na Kamati aya Siasa ya Momba na kukuta mgogoro wakiwatuhumu
viongozi wao kutumia vibaya mali ya chama ambayo ni mapato ya kodi ya Majengo.
Aliwataja
viongozi hao Mwenyekiti wa Kata ya Majengo Ndugu Daniel, Katibu wa Kata, Hemed
Steven na Katibu wa Fedha na uchumi ambapo pia kamati imeundwa ili kufuatilia
hali halisi iliyofujwa
0 maoni:
Post a Comment