Polisi Z,bar yapata msaada wa vitendea kazi


Bwana Zahor Mazrui akimkabidhi radio call kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Hamdan Omar.
Bwana Zahor Mazrui akimkabidhi radio call kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Hamdan Omar.

Jeshi la Polisi Zanzibar limesema litaendelea kuthamini jitihasa za wasamaria wema wenye nia ya kulipatia jeshi hilo msaada wa vitu mbali mbali kama vitendea kazi.
Kauli hio imetolewa na Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Hamdani Omar Makame, wakati alipokuwa akipokea msaada wa vitu mbali mbali kwa ajili ya kupeleka mbele harakati za Jeshi hilo kukabiliana na uhaifu wa aina mbali mbali Nchini huko makao makuu ya Polisi Ziwani Zanzibar.
Hamdan ameleza kuwa msaada huo uliotolewa na Katibu mtendaji wa jumuia ya Zanzibar Cheretable Society Bwana Zahor Mazrui umekuja kwa wakati muafaka kutokana na changa moto kadhaa zinazolikabili Jeshi la Polisi Zanzibar.
Akibainisha miongoni mwa Changamoto zinazolikabili Jeshi la Polisi Zanzibar Kamishna huyo amesema ni uhaba wa majengo sambamba na vitendea kazi.
Hivo ametoa wito kwa wasamaria wema wenye moyo kama wa Bwana Zahor Mazrui kujitokeza kwa ajili ya kulisaidia jeshi hilo ili liweze kufanya kazi zake kwa ufasaha.
Mara baada ya kukabidhi msaada huo wa Computer 10 radio call 30 printer 2 pamoja na calculate 90,Mkurugenzi mtendaji wa Zanzibar Cheretable Society Bwana Zahor Mazrui amesema ameamua kutoa msaada huo kwa jeshi la polisi ili wawe na nyenzo imara za kufanyia kazi ili kudhibiti wahalafu nchini.
Amebaisha kuwa msaada huo kwa jeshi hilo hautokuwa wa mwanzo na ataendelea kila pale anapopata wasaa kwani si jambo baya kusaidia Polisi.
”Wako watu wananishangaa sana kwa nini nawapa msaada jeshi la polisi lakini sitosita kwa sababu msaada utawafanya watende kazi zao kwa uadilifu”alieleza Bwana Mazrui.
Sambamba na hayo ametoa shukrani zake kwa jeshi hilo kupokea hicho kidogo alichokitowa na amewataka wasimchoke pale anapohitaji kutoa msaada mwengine zaidi.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment