Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
akiwa na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa
Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi, Mbunge wa Kongwa ambaye pia ni Naibu Spika
Job Ndugai, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Profesa
Juma Kapuya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa
Iyombe, akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa barabara ya
Mbande-Kongwa 16.5Km.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
wakwanza kushoto akiwa na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe
Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi pamoja na Mbunge wa
Kongwa ambaye pia ni Naibu Spika Job Ndugai wakifurahia mara baada ya
Rais kuweka jiwe la Msingi Ujenzi wa Barabara ya Mbande-Kongwa 16.5Km .
Waziri
wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipiga ngoma pamoja na
kikundi cha ngoma za asili cha Kibaigwa kabla ya Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuhutubia
mamia ya Wakazi wa Kibaigwa.
Sehemu ya barabara Mbande-Kongwa 16.5Km ambayo ujenzi wake umewekwa jiwe la Msingi.
Waziri
wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kulia akizungumza na
Mbunge wa Kibakwe ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa George Simbachawene huku Mbunge wa Kongwa
ambaye pia ni Naibu Spika Job Ndugai akishuhudia kushoto.
Waziri
wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katikati akizungumza na
Mbunge wa Kongwa ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) pamoja na Makamu
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Profesa Juma Kapuya(kulia)
kabla ya uzinduzi wa barabara ya Mbande-Kongwa 16.5Km.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
akizungumza na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
mara baada ya uzinduzi na ufunguzi wa barabara ya Mbande-Kongwa 16.5Km.
Viongozi
mbalimbali kutoka Wizara ya Ujenzi pamoja na Taasisi zake wakimsubiri
Rais Dkt. Jakaya Kikwete kuzindua rasmi mradi wa Ujenzi wa Barabara ya
Mbande-Kongwa 16.5Km. Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Ujenzi
0 maoni:
Post a Comment