ZAIDI ya kilo million nane za pamba
zinatarajiwa kununuliwa na chama kikuu cha ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU)
katika msimu wa mwaka
2014/2015,kutokana na baadhi ya makampuni ya kununua zao
hilo kujitoa kwa kudai kuwa soko la
dunia limeshuka hawatapata faida .
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Shinyanga meneja wa
SHIRECU mkoani hapa Joseph Mihangwa ,alisema mpaka sasa tayari wamenunua kilo
million 4.8 za pamba katika vituo vyake vyote huku wakitarajia kufikisha kilo
zaidi ya million nane ili kufiki lengo
walilokusudia.
Aisema mpaka sasa ni
asilimia 75 ya wakulima waliojitokeza kuuza pamba yao huku asilimia 25 wakisubiri kama soko litakuwa zuri ili wauze kwa bei
itakayo kuwa na tija kwao kwani bei iliyopo
hivi sasa ni shilingi 750 kwa kilo moja.
‘ Soko la dunia limekuwa baya kwa kuangalia bei
iliyopo hata hii ya shilingi 750 tunayonunua kutoka kwa
mkulima ni kubwa, hivyo tunanunua kwa matumaini huenda soko la
dunia bei yake ikawa nzuri baadaye ,kuna makampuni mengine yameacha ila sijajua
ni sababu gani kuu lakini wanadai soko la dunia limeshuka”alisema.
Akizungumzia suala la mizani Mihangwa alisema hakuna changamoto kwa upande wao kwani imekuwa ikisimamiwa na vyama vya msingi vya ushirika kwa usahihi ambapo vilivyopo vyama ni 480 ,vilivyochini ya SHIRECU ambapo kati ya hivyo 210 vimejiimarisha katika biashara na vilivyobaki vimeteteleka kutokana uchumi wake kutokuwa mzuri.
Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya
Shinyanga Ngassa Mboje akizungumzia zao hilo, alisema wakulima
wadogowadogo wamejitokeza kuuza ili kupata fedha na kukithi mahitaji ndani ya
familia ambapo baadhi ya wakulima wakubwa wakisubiri soko kuwa zuri wakati
msimu nao ukielekea mwisho.
Naye diwani wa kata ya Mondo wilayani Kishapu mkoani linapolimwa zao hilo kwa wingi John Ndama ,alisema wakulima wamekosa ujanja imebidi wauze kwa bei hiyo na kwamba kuna kampuni ya Villani ambayo ilianza kununua pamba kwenye baadhi ya maeneo kwa shilingi 800 kwa kilo moja .
Naye diwani wa kata ya Mondo wilayani Kishapu mkoani linapolimwa zao hilo kwa wingi John Ndama ,alisema wakulima wamekosa ujanja imebidi wauze kwa bei hiyo na kwamba kuna kampuni ya Villani ambayo ilianza kununua pamba kwenye baadhi ya maeneo kwa shilingi 800 kwa kilo moja .
Baadhi ya wakulima wa zao la pamba mkoani
Shinyanga akiwemo Maduhu Shija na Bernadetha Joshua
walisema wakulima wamekubali kuuza kwa bei ya shilingi 750 kwa kilo,
kutokana na changamoto kubwa ndani ya familia kukosa kipato huku wakiunga mkono baadhi ya
makampuni kujitoa kwani wameona wanapata hasara.
0 maoni:
Post a Comment