Saed Kubenea
----
Ndugu waandishi wa habari,Natumaini mna taarifa kwamba tangu Ijumaa iliyopita, nimefungua shauri Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam, kupinga kinachofanywa na Bunge Maalum la Katiba. Shauri hilo, limesajili kwa Na.28 la mwaka 2014.
Katika kesi hiyo, nimeomba Mahakama Kuu itoe tafsiri sahihi juu ya mamlaka ya Bunge Maalum la Katiba, chini ya kifungu cha 25 (1) na (2) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 ya mwaka 2011.
Aidha, nimewasilisha maombi madogo nikiomba Mahakama kutoa zuio la muda la kusimamisha Bunge Maalum la Katiba, wakati tukisubiri uamuzi wa kesi ya msingi. Maombi ya zuio yamepangwa kutajwa tarehe 4 Septemba na kesi ya msingi itatajwa 15 Septemba 2014.
Ndugu waandishi wa habari,
Tangu kuripotiwa kufunguliwa kwa shauri hili mahakamani, yapo mengi yaliyosemwa. Wapo walionipongeza na kunifariji. Wapo walionitia moyo na kuniomba nisirudi nyuma. Wapo walionidhihaki na kunikatisha tamaa. Wapo walionitisha.
Lakini wapo walioahidi kuniombea kwa Mwenyezi Mungu ili jambo hili kubwa nililolifanya kwa maslahi ya taifa langu, niweze kulifikisha mwisho nikiwa mzima na mwenye amani.
Ninafahamu jukumu hili nililolibeba ni zito sana. Linaweza likasababisha baadhi ya watu kukosa posho ikiwa mahakama itaridhia ombi langu la usitishaji wa Bunge la Katiba. Linaweza kunitenganisha na baadhi ya ndugu na marafiki zangu. Linaweza kuhatarisha hata maisha yangu.
0 maoni:
Post a Comment