Afisa
ufundi wa kilimo cha mboga kutoka TAHA Bw. Abdon akiwaelekeza wakulima
kuhusu mbinu bora za uoteshaji wa miche ya mboga kwenye trei maalumu
katika mahadhimisho ya siku ya wakulima shambani kwa wakulima wa kijiji
cha Mferejini-Machame katika wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro.
Wakulima wakimsikiliza mtaalamu wa masuala ya mbolea na viatilifu kutoka kampuni ya Triachem Bi.Baby Nkassa wakati akizungumzia suala zima la matumizi fasaha ya mbolea na viatilifu kwenye mazao
Katibu
tawala wa Wilaya ya Hai Bi. Zuhura Chikira ambaye alikuwa mgeni rasmi,
akisiliza maelezo kutoka kwa mtaalamu wa kilimo cha mboga kutoka TAHA
Bw. Giliard Daniel katika mahadhimisho ya siku ya wakulima shambani kwa
wakulima wa kijiji cha Mferejini-Machame katika wilaya ya Hai Mkoa wa
Kilimanjaro.
Shamba mfano namba 1
Shamba mfano namba 2
Mzee Shabani Shoo akizungumza na wakulima (hawapo pichani)kuhusu mbinu alizofundishwa na wataalamu
wa TAHA na kuweza ukuaji bora wa zao lake la kabeji ikiwa ni pamoja na ongezeko la idadi ya mazaokutoka kabeji 4000-18000
Wakulima
wa Kijiji cha Silversand-Machame wakifuatilia mafunzo ya namna bora ya
uandaaji wa udongo kwa ajili ya kuotesha miche ya mbogamboga
Wakulima waliohudhuria mafunzo ya kilimo cha mboga katika siku ya wakulima shambani wakifuatilia hotuba kutoka kwa mgeni rasmi
Wakulima wakifatilia maelezo kutoka kwa mtaalamu wa kilimo cha mboga mboga kutoka TAHA Bw.Collins Okiyawakati wa mafunzo hayo
Asasi
ya sekta binafsi ya wakulima wa mboga mboga,Matunda, maua, viungo na
mbegu zake imehadhimisha siku ya wakulima shambani kwa wakulima wa
kijiji cha Mferejini-Machame katika wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro.
Maadhimisho
hayo yamekuwa yakifanyika kila baada ya Mwezi mmoja mpaka miwili ili
kutoa fursa kwa wananchi kujifunza mbinu bora za kilimo cha mazao ya
‘horticulture’ ikiwa ni sambamba na kujifunza mbinu fasaha za kilimo
biashara.
0 maoni:
Post a Comment