* Asaini kitabu cha maombolezo ya Waziri Mkuu wa zamani
WAZIRI
MKUU Mizengo Pinda ametumua salamu za rambirambi kwa Serikali ya Ireland
kufuatia kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani wa nchi hiyo, Bw.
Albert Reynolds.
Hayati
Reynolds ambaye amefariki akiwa na miaka 81, alikuwa Waziri Mkuu wa nane
wa nchi hiyo kwa miaka mitatu kuanzia mwaka 1992. Atakumbukwa kwa
kuanzisha mchakato wa kuleta amani Ireland Kaskazini dhidi ya kundi la
IRA.
Waziri
Mkuu Pinda ambaye aliwasili jana (Alhamisi, Agosti 28, 2014) jijini Dar
es Salaam akitokea Dodoma, alikwenda moja kwa moja ubalozi wa Ireland na
kusaini kitabu cha maombolezo cha kiongozi huyo.
Katika
salamu za rambirambi, Waziri Mkuu amemwelezea Bw. Reynolds kuwa ni
kiongozi atakayekumbukwa kwa kuleta amani duniani na misaada ya
kimaendeleo nchini Tanzania.
“Kwa
niaba ya Serikali ya Tanzania, ninawapa pole sana kwa kufiwa na Kaka
yetu na ndugu yetu, Waziri Mkuu wa zamani wa Ireland, Albert Reynolds.
Tunashirikiana nanyi katika kipindi hiki cha majonzi. Tutaendelea
kumkumbuka kwa kazi nzuri alizofanya kwa nchi yetu na duniani. POLENI
SANA KWA MSIBA HUU MKUBWA,” inasomeka sehemu ya salamu za rambirambi
alizotoa Waziri Mkuu.
Akipokea
salamu hizo, Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Bibi Fionnuala Gilsenan
alimshukuru Waziri Mkuu Pinda kwa kufika ubalozini hapo na kuwapa pole
kwa kifo cha Waziri Mkuu wao wa zamani.
“Tutamkumbuka
kiongozi wetu kwa mambo mengi aliyoifanyia nchi yetu… Tunafarijika kwa
salamu hizi za rambirambi. Tutafikisha kitabu hiki cha salamu za
rambirambi kwa familia yake, naamini nao watafarijika sana,” alisema
Balozi Gilsenan.
Balozi Gilsenan alimweleza Waziri Mkuu kwamba kitabu cha maombolezo kitafungwa leo.
0 maoni:
Post a Comment