DRC:JENERALI EMMANUEL LOMBE MKUU WA MAJESHI KIVU KASKAZINI.

Jeshi la Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo  FARDC limemteua kamanda mpya kuchukua nafasi ya General Lucien Bahuma Ambamba aliyefariki mwishoni mwa juma lililopita Afrika Kusini.

Brigedia jenerali Emmanuel Lombe,ndiye kamanda mpya wa mkoa wa nane wa kijeshi 8 jimboni kivu kaskazini ambapo mara baada ya kuteuliwa aliwasili na kuanza kazi jumanne wiki hii anakutana na maafisa wa jeshi la FARDC na Askari wa kulinda Amani MONUSCO mjini Goma.

Jenerali Lombe pia amepewa jukumu la kuliongoza jeshi jimboni humo katika opereshini maarufu kwa jina la "Sokola"dhidi ya waasi wa Uganda wa ADF- nalu mjini Beni ambapo opereshini hiyo inatarajiwa kuendelea kwa msaada wa MONUSCO

Hata hivyo kiongozi huyo mpya atakabiliana na tatizo la makundi yenye kumiliki silaha katika maeneo mengine ya kivu kaskazini ikiwemo walikale,Masisi,Rutshuru,Rubero na Beni ambapo makundi haya bado hayajaridhia mchakato wa kuwasambaratisha ,kuwapokonya silaha,na kuwaunganisha na jamii zao kulinganas na mpango wa DDRR Wa serikali ya Kinsasha

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment