HII IMEKAA VIBAYA !!! POLISI WAKUMBWA NA KASHFA NYINGINE YA KUWATESA NA KUWADHALILISHA WATUHUMIWA TANZANUA.


Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Jaji Amiri Manento.
 
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imesema Jeshi la Polisi  limekuwa likitumia nguvu kubwa katika kuwashughulikia watuhumiwa wa kesi  mbalimbali nchini.

Pia imesema nguvu, ambayo imekuwa ikitumika kuwashughulikia watuhumiwa ni pamoja na kuwatesa, kuwadhalilisha, kuwabambikia kesi, kuwekwa kuzuizini kwa muda mrefu, bila kufikishwa mahakamani pamoja na mazingira magumu ya dhamana jambo linalokiuka haki za binadamu.

Imesema vitendo hivyo vimekuwa vikifanywa na polisi wakati wa kufanya mahojiano na watuhumiwa kwa kuwashinikiza kukiri makosa na kusababisha kuwa na idadi kubwa ya mahabusu na wafungwa na kuisababishia mzigo mkubwa serikali.

Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Kisheria wa Ttume hiyo, Nabol Assey, alisema hayo  wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Alisema tafiti zilizofanywa na tume hiyo kwa nyakati tofauti hivi karibuni, zinaonyesha kuwa pia yamekuwapo malalamiko kutoka kwa watuhumiwa na wafungwa wanaolalamikia kubambikizwa kesi na polisi.

“Mara nyingi ukamataji unaofanywa na vyombo vya dola, hususan Jeshi la Polisi mara nyingi, unakiuka haki za binadamu. Tafiti zinaonyesha kwamba, kumekuwapo na matumizi ya nguvu kupita kiasi dhidi ya watuhumiwa, ambayo huambatana na vitendo vya utesaji wa watuhumiwa, ambao unafanywa wakati wa mahojiano kwa lengo la kuwashinikiza kukiri makosa,” alisema Assey.

Aliongeza: “Hii inatokana na kukosekana kwa weledi kutoka kwa polisi wenyewe na uelewa mdogo wa sheria, kanuni na utaratibu zinazohusiana na haki za binadamu katika mfumo wa haki jinai.”CHANZO: NIPASHE
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment