Ofisi ya OCD ikiwa imebolewa na FFU FFU wakisimamia zoezi la ubomoaji |
Zoezi la ubomoaji nyumba likiendelea Kituo cha polisi cha wilaya kikiwa kimebolewa Wananchi wakishuhudia tukio la aina yake-picha zote na Hilali Alexander Ruhundwa-Malunde1 blog-Kagera |
Katika hali ya kushangaza na iliyowaacha vinywa wazi wananchi, askari wa kutuliza ghasia F.F.U wamesimamia
zoezi la kubomoa kituo cha polisi cha wilaya pamoja na nyumba
wanazoishi askari polisi wilaya ya Karagwe mkoani Kagera kupisha ujenzi
wa barabara yenye urefu wa km. 59.1 toka Kyaka wilayani Missenyi hadi
Bugene wilayani Karagwe kwa kiwango cha lami.
Ofisi
ya mkuu wa jeshi la polisi (OCD) pamoja na nyumba za makazi ya askari
polisi vimebomolewa na kampuni inayojenga barabara hiyo China Henan
International Group (CHICO) ndiyo iliyoendesha zoezi hilo la bomoabomoa
chini ya usimamizi wa F.F.U baada ya maaskari polisi kudaiwa kugoma
kuhama.
Ni
tukio lililovuta makini ya wengi huku minong'ono ikitawala ya ukosoaji
wa kauli ya polisi "Utii wa sheria bila shuruti", wakihoji maana yake
kwani nao (polisi) wamekaidi kutii sheria hadi kuletewa F.F.U
kuwashughulikia endapo wangejaribu kuleta fujo.
Meneja
wa TANROADS mkoa wa Kagera John Kalupare alipopigiwa simu kuelezea
tukio hilo amesema yupo safarini Dar es Salaam na asingeweza kuzungumzia
suala hilo.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi mkoa wa Kagera (RPC) Henry Mwaibambe alipopigiwa
simu juu ya tatizo hilo, simu yake imeita bila kupokelewa.
Mmoja
wa maofisa wa TANROADS aliyekuwa anasimamia zoezi hilo ambaye
hakupenda jina lake litajwe, amesema kuwa wao wanaonesha mipaka ya
barabara na polisi wanabomoa nyumba zao.
"Sisi
TANROADS tunaonesha mipaka ya barabara na polisi wanabomoa nyumba zao
na kituo chao hivyo waulize wao kwanini ubomoaji unafanywa chini ya
ulinzi mkali". amesema.
Hata
hivyo zoezi hilo limeingiwa na dosari baada ya kundi la nyuki kutokea
na kuwashambulia wabomoaji, maaskari na mashuhuda wa tukio hilo huku
dereva akilazimishwa na wachina kuendelea na ubomoaji licha ya kung'atwa
na nyuki hao.
Ni
tukio linaloshangaza na kuitia doa serikali kwa jeshi la polisi lenye
dhamana ya kulinda usalama na raia ambalo daima huhubiria raia utii wa
sheria bila shuruti sasa linaenda kinyume hadi kuletewa F.F.U
kulisimamia.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi wilaya Karagwe hakupatikana kuzungumzia sakata hilo
ambapo inadaiwa kuwa bomoabomoa hiyo itaigharimu halmashauri hiyo
baadhi ya ofisi zitakazobomolewa ikiwemo ofisi za wabunge wa majimbo ya
Karagwe na Kyerwa.
Na Hilali Alexander Ruhundwa-Malunde1 blog-Kagera
0 maoni:
Post a Comment