Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar ambaye pia ni KAtibu Mkuu wa CUF akiwasili mjini Mwanza.
Katibu mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad akihutubia mkutano wa hadhara Wilayani Kwimba mkoa wa Mwanza jana.
Na Khamis Haji
Katibu
Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amewahimiza
wananchi wa mkoa wa Mwanza kujiweka tayari kukipa talaka Chama cha
Mapinudizi na waunge mkono Umoja wa vyama unaotetea Katiba ya Wananchi
(Ukawa) katika uchaguzi wa 2015 uwaletee mabadiliko ya kimaisha.
Maalim
Seif ameyasema hayo alipokuwa akihutubia katika mikutano ya hadhara
katika vijiji vya Ngudu na Hungumalwa Wilaya ya Kwimba, akiwa katika
zaiara ya siku nne, ambapo pia amefuatana na viongozi waandamizi wa
CHADEMA wa mkoa wa Mwanza.
Maalim Seif alisema katika kipindi cha miaka 53 tangu nchi ilipopata uhuru kila siku zinavyokwenda mbele hali za maisha ya wananchi zinazidi kuwa mbaya, kutokana na nchi kukosa uongozi bora chini Chama cha Mapinduzi.
“Ujumbe
wetu kwenu ni kuwa CCM imeshalewa madaraka haiwezi tena kuwaletea
mabadiliko ya kimaisha, kipeni talaka CCM na mchague vyama vyenye uwezo
wa kuwaletea maendeleo”, alisema Katibu Mku wa CUF.
Alisema
uthibitisho wa CCM kukosa uwezo wa kuwaletea mabadiliko ya kimaisha
wananchi ni namna wanavyo vuruga mchakato wa kupata Katiba Mpya ambao
wananchi wa Tanzania
Bara na Zanzibar walitarajia uweke misingi bora ya maisha yao, ikiwemo
matumizi ya maliasili za ardhi, madini, kilimo, elimu bora na utawala
bora kwa jumla.
Maalim
Seif alisema CCM wamebadilisha maoni ya wananchi yaliyowasilishwa na
Tume ya Mbadiliko ya Katiba chini ya Jaji Mstaafu Warioba, maoni ambayo
msingi wake ni mfumo wa Serikali tatu baada ya wananchi hao kubaini ndio wenye maslahi kwao.
Katibu
Mkuu huyo wa CUF alisema badala yake CCM kimepindua maoni hayo bila ya
kujali fedha nyingi zilizotumika, lengo lao likiwa ni kulinda maslahi ya
wachache na kupuuza shida zinazowakabili Watanzania ambao wameshaona
mfumo wa Serikali mbili hauwafai tena.
Alieleza
kuwa wanafanya hivyo kuendeleza ufisadi unaofanywa na baadhi ya
viongozi wa chama hicho kama ule wa kuiba fedha nyingi za wananchi na
kwenda kuzificha katika mabenki ya nje kama nchini Uswis.
“Vyama
vya CUF, CHADEMA na NCCR Mageuzi vina viongozi makini wenye uwezo wa
hali ya juu na vimedhamiria kikweli kuwaletea mabadiliko ya kimaisha
wananchi wote wa Tanzania, bila ya ubaguzi, kama inavyofanyika chini ya
CCM”, alisema.
Naye,
Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Ilemela, Greyson Wanzagi Warioba
akihutubia katika mkutano wa Ngudu alisema CCM imejidhihirisha wazi
hakikuwa upande wa wananchi kwa miaka yote tangu kupatikana uhuru
kutokana na kitendo chao cha kujifungia Dodoma na kupindua maoni ya
wananchi wa Tanzania.
Alisema
chama hicho kinajali maslahi yao binafsi, na Umoja wa Kutetea maoni ya
Wananchi (Ukawa) utaendela kufichua maovu wanayofanya, ili wananchi
wayaelewe na wakikatae katika uchaguzi mkuu ujao.
Naibu
Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mawasiliano ya Umma wa CUF, Hamis
Kambaya alisema Serikali ya CCM haiwajali wananchi wa Kanda ya Ziwa
kutokana na kitendo cha kuwapatia wananchi hao mbegu zisizofaa za zao la
Pamba.
Mbali
na hilo alisema bei ya zao hilo hivi sasa ni ya chini ambayo haiwezi
kumsaidia mkulima anayekabiliwa na hali duni ya maisha na kumfaya
ashindwe kupata mlo kamili wa siku, mbali na huduma nyengine kadhaa wa
kadhaa muhimu za kijamii zinazomkabili.
Mwenyekiti
wa Wanawake wa CHADEMA katika mkoa wa Mwanza, Suzan Masele alisema
umefika wakati wanawake waepuka kulaghaiwa kwa Khanga na Vitenge
kunakofanywa na viongozi wa CCM wakati wa uchaguzi kwa sababu mambo hayo
tayari yamepitwa na wakati.
0 maoni:
Post a Comment