Kikosi cha Mabingwa watetezi wa Ligu Kuu ya Grand Malt mwaka jana Timu
ya KMKM, wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo wao wa kwanza
kuanza na timu ya Malindi uliofanyika uwanja wa Amaan timu ya KMKM
imeshinda 2--1 dhidi ya timu ya Malindi
Kikosi cha timu ya Malindi kilicholazimishwa kukubali uteja kwa timu ya KMKM kwa kukubali kufungwa mabao 2--1.
Mshambuliaji wa timu ya Malindi Haji wa Haji akimpita beki wa timu ya
KMKM Mwinyi Haji katika mchezo wa Ligi Kuu ya Grand Malt raundi ya
kwanza mchezo uliofanyika uwanja wa amaan, timu ya KMKM imeshinda mchezo
huo 2--1.Haji wa Haji mfungaji wa timu ya Malindi bao la kufutia
machozi katika dakika ya 84 ya mchezo huo kipindi cha pili.
Mshambuliaji wa timu ya Malindi Haji
wa Haji akiruka kihuzi cha beki wa timu ya KMKM, katika mchezo wa ligi
kuu uliofanyika uwanja wa amaan. timu ya KMKM imeshinda mchezo huo
2--1.
Golikipa wa timu ya KMKM Mudathir Khamis akidaka mpira wakati wa mchezo
wao wa ligi kuu ya grand malt na timu ya Malindi ul;iofanyika uwanja wa
Amaan jana.
Wachezaji wa timu ya KMKM na Malindi wakiwania mpira ukiwa juu kulia
mchezaji wa timu ya Malindi Daud Suleiman na kushoto mchezaji wa KMKM
Ibrahim Khamis.
Beki wa timu ya KMKM Khamis Ali kulia akijaribu kumzuiya mshambuliaji wa
timu ya Malindi Abdulsalam Othman, wakati wa mchezo huo wa ligi kuu ya
grand malt iliofanyika uwanja wa amaan timu ya KMKM imeshinda 2--1.
Ads by 1ClickMovie-Download1.1Ad Options
0 maoni:
Post a Comment