Mapambano dhidi ya Ebola yapungua Afrika


Mkuu wa shirika la madawa la kimataifa la madaktari wasio na mipaka MSF, Joanne Liu ameuambia Umoja wa Mataifa kuwa mapambano dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa ebola Afrika Magharibi yamepungua.
Amesema viongozi duniani wameshindwa kutafutia ufumbuzi wa ugonjwa huo hatari katika historia.
Amesema pia kumekua na Madaktari wachache na katika vituo vilivyotengwa vya kutibu wagonjwa wameendelea kufa. Mratibu wa umoja wa mataifa anayehusika na majanga David Nabarro, amesema watafanya wawezalo kuongeza wafanyakazi wengi wa afya ili kupambana na ugonjwa huu. ( zaidi ya watu mia tano wamekufa kutokana na ugonjwa huo ) na wataalam wa afya wameonya kwamba maelfu ya watu wanauwezekano wa kuambukizwa ugonjwa huo kwa wiki chache zijazo..
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment