Mapambano dhidi ya wanamgambo wa IS yapamba moto


Image result for wanamgambo wa IS PixMarekani na washirika wake wa kiarabu wameanzisha mashambulizi kutoka angani na baharini dhidi ya wanamgambo walio na itikadi kali wa Dola la Kiislamu IS nchini Syria, na kufungua mkabala mpya katika vita  dhidi ya  kundi hilo la kikatili la wapiganaji wa jihadi. Uongozi wa juu wa jeshi la Marekani umesema nchi za Bahrain, Jordan, Saudi Arabia, Qatar na nchi ya falme za kiarabu zimeungana na Marekani katika mashambulizi hayo. Mashambulizi hayo yaliyaharibu au kuviangamiza vituo vingi vilivyolengwa vya wapiganaji hao katika ngome zao  Kaskazini mwa Syria na karibu na mpaka wa Iraq , yakiwemo maeneo ya mafunzo, taasisi za mawasiliano na magari ya kivita.  Mashambulizi ya angani yanayoongozwa na Marekani nchini Syria yameleta sura mpya katika vita vyake dhidi ya wanamgambo wa IS wanaodhibiti maeneo mengi nchini Iraq na Syria na kutangaza utawala wa sheria ya kiislamu
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment