Ufaransa yasema haitozungumza na kundi la wanamgambo

Image result for Ufaransa PixWaziri Mkuu wa Ufaransa Manuel Falls ameapa kwamba hakutakuwa na majadiliano yoyote na kundi la Algeria linalofungamanishwa na wanamgambo walio na itikadi kali wa dola la Kiislamu, lililokiri kumteka nyara raia wa Ufaransa, na kusisitiza kuwa Ufaransa itaendelea na mashambulizi yake ya angani dhidi ya kundi hilo. Kundi hilo la Jund al-Khalifa au wanajeshi wa utawala wa sheria za kiislamu, wameahidi katika ujumbe wao kwa njia ya Video kwamba watamuua mateka huyo Herve Pierre Gourdel, saa 24 zijazo ikiwa Ufaransa haitositisha mashambulizi yake dhidi ya kundi la IS nchini Iraq. Ijumaa iliopita  Ufaransa ilifanya shambulizi lake la kwanza la angani nchini Iraq lakini ikasema haitofanya mashambulizi kama hayo nchini Syria
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment