1.Khardung La, India
Barabara 12 hatari zaidi duniani
Chaneli ya National Geographic pamoja na watu wanaotoa tuzo za Guiness wamekubali hii ni moja kati ya barabara ndefu zaidi duniani! Unapopita kwenye hii barabara lazima macho yawe madirishani kuangalia mawe yanayoporomoka kabla ya kuendelea na safari.
2. Guoliang Tunnel, China
Barabara 12 hatari zaidi duniani
Barabara hii ya mita 1200 ambayo imepasuliwa kwenye mlima kama inavyoonekana hapo!
3. Dalton Highway, Alaska
Barabara 12 hatari zaidi duniani
Inafahamika kama moja kati ya barabara zenye baridi kali zaidi na pweke duniani kwani inaweza ikapita gari moja tu kwa mwezi, kama unavyoiona baridi lake sio la kitoto, Hebu fikiria mnapita hapo harafu gari inapata hitilafu.
4. Eshima Ohashi Bridge, Japan
Barabara 12 hatari zaidi duniani
Barabara hii ilivyokaa kama ile michezo ya rollercoaster ambapo mnakuwa kama kwenye treni inayopita kwenye njia maalumu! Ilitengenezwa hivyo ili kuwezesha meli kupita kirahisi kwa chini.
5. Atlantic Ocean Road, Norway
Barabara 12 hatari zaidi duniani
Watalii wanapendelea barabara hii kutokana na mawimbi ya bahari yanavyongonga kwenye vizuizi vya barabara hii.
6. Zoji La, India
Barabara 12 hatari zaidi duniani
Barabara hii ilitengenezwa kuunganisha mji wa Ladakh na Kashmir, Licha ya kuwa na mawemawe ni nyembamba balaa! Si hivyo tu pia kupishana pamoja na mifugo wakati unaendesha gari yako ni jambo la kawaida sana.
7. Hana, Hawaii
Barabara 12 hatari zaidi duniani
Imefungwa kutokana na kuteleza mno, barabara hii nyembamba ipo katika kisiwa cha Maui.
8. Kolima, Russia
Barabara 12 hatari zaidi duniani
Barabara hii inafahamika kwa jina la utani kama “Barabara Kifo” sehemu ya barabara hii ilitengenezwa na wafungwa. Ujenzi ulianza mwaka 1932, ila haukukamilika mpaka 1953. Inatisha kidogo!
9. Yungas, Bolivia
Barabara 12 hatari zaidi duniani
Ilitengenezwa kwenye pembe za mlima, barabara hii inafahamika kama moja kati ya hatari duniani. Kila mwaka inaua watu 200 – 300.
10. Le Passage du Gois, France
Barabara 12 hatari zaidi duniani
Barabara hii inafunguliwa kwa masaa kadhaa kisha kufungwa kutokana na maji ya mto kujaa kwenye barabara hiyo.
11. Caucasus, Russia
Barabara 12 hatari zaidi duniani
Wembamba wa barabara hii unaweza ukakutisha lakini watu wamekuwa wakifurahia kupita hapa na kuangalia muonekano mzuri wa milima.
12. Transfagarasan, Romania
Barabara 12 hatari zaidi duniani
Ingawa inaweza ikawa siyo barabara ndefu duniani, lakini inafahamika kuwa tishio kutokana na kona nyingi ilizokuwa nazo.
from Blogger http://ift.tt/2kRefq4
via IFTTT
0 maoni:
Post a Comment